-
Iran yakosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ubabe wa Marekani
Oct 15, 2020 04:21Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema uchukuaji hatua za upande mmoja wa Marekani ndilo tishio kuu kwa haki za binadamu duniani, huku akikosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ubabe huo wa Washington.
-
Zarif: Uwepo wa vikosi ajinabi Mashariki ya Kati unashadidisha matatizo
Oct 15, 2020 00:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa uwepo wa wanajeshi ajinabi katika eneo la Mashariki ya Kati ni tete na unashadidisha matatizo mbalimbali. Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan.
-
Zaidi ya wagonjwa 4,800 wapya wa corona wagunduliwa Iran
Oct 14, 2020 09:11Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ametangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa wapya elfu nne na mia nane (4,800) wa COVID-19 wamegunduliwa humu nchini katika kipindi cha saa 24 zlizopita.
-
Iran yachukua uwenyekiti wa Kundi la 24
Oct 14, 2020 04:15Gavana wa Benki Kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kundi la 24 (G24) katika kikao cha mawaziri wa fedha na magavana wa benki wa nchi wanachama kilichofanyika kwa njia ya intaneti.
-
Ndoto za alinacha za Trump za kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Oct 13, 2020 22:53Rais Donald Trump wa Marekani akiwa na lengo la kujijengea nafasi nzuri wakati huu wa kukaribia uchaguzi nchini humo, anahitajia kutoa madai ya kufanikiwa katika sera za kigeni za nchi hiyo hasa kuhusiana na Iran.
-
Namaki: Iran inapambana na vikwazo na corona kwa wakati mmoja
Oct 13, 2020 08:08Waziri wa Afya wa Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapambana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na virusi vya corona kwa wakati mmoja."
-
El-Baradei: Mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi ya Marekani dhidi ya Iran yamefeli
Oct 13, 2020 04:18Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amekosoa vikali sera ya mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, mashinikizo hayo yamegonga mwamba.
-
Iran yataka Saudi iwajibishwe kwa shughuli zake za siri za nyuklia
Oct 13, 2020 04:14Mwakilishi wa Iran katika Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ametoa mwito wa kubebeshwa dhima Saudi Arabia kutokana na kuendesha shughuli zake za nyuklia kwa siri na kificho.
-
Iran: Marekani ni kidhabi kwa kudai vikwazo vipya havilengi sekta ya afya
Oct 11, 2020 08:41Waziri wa Afya wa Iran amelaani hatua ya Marekani ya kuliwekea vikwazo shadidi taifa hili na kubainisha kuwa, utawala wa Washington umekubuhu kwa kusema uwongo, kwa madai yake kuwa vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu havilengi sekta ya afya na tiba.
-
Trump anaitusi Iran kwa sababu amefeli katika njama zake dhidi ya Iran
Oct 11, 2020 04:31Mwenyekiti wa Baraza la Kistratijia la Sera za Kigeni la Iran, Dkt. Kammal Kharrazi, ametoa kauli kufuatia matamshi yaliyojaa matusi ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kusema, Trump amepandwa na hasira baada ya kufeli njama zake dhidi ya Iran.