Zarif: Uwepo wa vikosi ajinabi Mashariki ya Kati unashadidisha matatizo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64020-zarif_uwepo_wa_vikosi_ajinabi_mashariki_ya_kati_unashadidisha_matatizo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa uwepo wa wanajeshi ajinabi katika eneo la Mashariki ya Kati ni tete na unashadidisha matatizo mbalimbali. Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 15, 2020 00:52 UTC
  • Zarif: Uwepo wa vikosi ajinabi Mashariki ya Kati unashadidisha matatizo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa uwepo wa wanajeshi ajinabi katika eneo la Mashariki ya Kati ni tete na unashadidisha matatizo mbalimbali. Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan.

Katika mazungumzo hayo, Toshimitsu Motegi Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan na Muhammad Javad Zarif wamefanya mashauriano kuhusu matukio ya kimataifa, kieneo na kuhusu uhusiano wa pande mbili. 

Zarif aidha ameashiria ulazima wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kustafidi na rasilimali zake za fedha za kigeni zilizoko Japan na kulaani vizuizi vilivyo kinyume cha sheria vinavyotekelezwa na serikali ya Marekani katika uwanja huo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aidha ameitaja hatua ya Marekani ya kuzuia kununua madawa na chakula kwa ajili ya wananchi wa Iran kuwa ni jinai dhidi ya ubinadamu.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, anataraji serikali ya Japan itazuia kutekelezwa hatua hiyo iliyo kinyume cha sheria ya Marekani katika fremu ya majukumu ya pamoja ya nchi mbalimbali katika kutekeleza maazimio ya Baraza la Usalama likiwemo  azimio nambari 2231 la Umoja wa Mataifa. Kwa upande wake Toshimitsu Motegi amesisitiza kuimarisha uhusiano katika mapambano dhidi ya corona na kutumwa suhula za kitiba kwa kutumia vyanzo vya fedha vya Iran na kueleza kuwa msimamo wa Japan wa kufanya juhudi za kuhakikisha kuwa eneo la mashariki ya Kati linakuwa na amani haujabadilika. Motegi amesema, Japan  inaunga mkono mapatano ya JCPOA. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan,  Toshimitsu Motegi