-
Zarif: Iran haitapoteza muda kufanya mazungumzo na US
Oct 02, 2018 04:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran katu haitafanya mazungumzo na Marekani madhali Washington itaendelea kukataa kukumbatia uhalisia wa mambo na muamana.
-
Qassemi: Msimamo wa Ulaya unakidhi maslahi ya Iran katika JCPOA
Oct 01, 2018 11:17Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumekuwa na hali ya kukaribiana misimamo ya Iran na Ulaya kuhusiana na kukidhiwa maslahi ya Tehran baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi.
-
Walid al Mualim: Kuwepo washauri wa Kiirani Syria ni kwa mujibu wa sheria
Sep 30, 2018 10:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesisitiza kuwa washauri wa kijeshi wa Iran wapo nchini humo kwa mujibu wa sheria kinyume na Marekani ambayo iko kijeshi nchini humo kinyume cha sheria.
-
Sergey Lavrov: Kuondoka mashirika ya Ulaya nchini Iran ni kosa kubwa
Sep 29, 2018 21:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, sambamba na kuunga mkono ubunifu wa Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa mabadilishano ya kifedha pamoja na Iran, amesema kuwa kuondoka mashirika ya Ulaya nchini Iran, ni kosa kubwa.
-
Ibrahim al-Jaafari: Madai ya Netanyahu juu ya uwepo wa askari wa Iran nchini Iraq ni uongo mtupu + Video
Sep 29, 2018 11:43Ibrahim al-Jaafari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq ametupilia mbali madai yasiyo na msingi wowote ya Waziri Mkuu wa utawala Haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu juu ya uwepo wa askari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq na kuongeza kuwa, maneno hayo ni uongo mtupu.
-
Mkutano wa US na nchi za Kiarabu wa kuunda muungano dhidi ya Iran
Sep 29, 2018 04:44Marekani hapo jana ilikuwa mwenyeji wa wanadiplomasia wa ngazi za juu wa nchi za Kiarabu katika kikao kilichojadili mpango wa kuundwa eti muungano wa kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Sayyid Araqchi: Kuzungumza na Iran kwa lugha ya vitisho hakuna faida
Sep 28, 2018 23:14Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa ameihutubu serikali ya Marekani akiiambia kwamba, kuzungumza na taifa la Iran kwa lugha ya vitisho katu hakuwezi kuwa na faida si sasa hivi tu bali hata katika siku za usoni.
-
Ayatullah Movahhedi Kermani: Lengo la maadui ni kuleta hali ya kukatisha tamaa kwa wananchi
Sep 28, 2018 11:07Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, lengo la njama kubwa za maadui na hatua yao ya kuanzisha vita vya kila upande vya kiuchumi na kisaikolojia ni kuwakatisha tamaa na kuwachokesha wananchi wa Iran ambao daima wamekuwa na mahudhurio makubwa katika medani za masuala ya Iran ya Kiislamu.
-
Baraza Kuu la UN; uwanja wa kukejeliwa Trump, jukwaa la mazingaombwe ya Netanyahu
Sep 28, 2018 10:44Kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimefanyika, huku walimwengu wakijionea igizo jengine la usanii wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel; utawala ambao una mamia ya vichwa vya nyuklia, silaha ambazo ni tishio na hatari kwa usalama wa dunia. Hata hivyo kutokana na kuungwa mkono na Marekani, utawala huo khabithi hauwajibiki kwa taasisi yoyote ile duniani.
-
Iran: Israel itajuta kwa kuwaunga mkono magaidi na kuishambulia Syria
Sep 27, 2018 12:39Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kuendelea kuzishambulia ngome za jeshi la Syria na waitifaki wake na kusisitiza kuwa, Tel Aviv itakabiliwa na jibu kali iwapo haitasitisha uvamizi wake na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu.