-
Iran yakanusha madai ya kuomba kufanya mazungumzo na Trump
Sep 21, 2018 23:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataja kama kichekesho madai kwamba taifa hili limeomba kufanya mkutano na Rais Donald Trump wa Marekani.
-
Iran yatuma salamu za rambirambi kwa Tanzania kufuatia ajali ya kivuko, Mwanza
Sep 21, 2018 09:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa taifa na serikali ya Tanzania kufuatia ajali ya kuzama kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Vctoria huko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
-
Marekani, Saudia, UAE na Israel zatengwa katika njama zao dhidi ya Iran katika IAEA
Sep 20, 2018 01:45Marekani na waitifaki wake wanaoipiga vita Iran wametengwa vibaya katika mkutano mkuu wa Wakala wa Kimataifa ya Nishati ya Atomiki IAEA.
-
Maafikiano ya Sochi na uungaji mkono wa Iran kwa utumizi wa diplomasia kutatua kadhia ya Idlib
Sep 19, 2018 09:48Makubaliano yaliyofikiwa mjini Sochi kati ya Russia na Uturuki kuhusu kadhia ya eneo la Idlib lililoko kaskazini magharibi mwa Syria baada ya kikao kilichofanyika mjini Tehran kati ya marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia na Uturuki yamekaribishwa na kuungwa mkono na Iran. Maafikiano hayo ni ishara ya mwendelezo wa njia athirifu za kidiplomasia.
-
Qassemi: Uhusiano wa Iran na Afrika umesimama juu ya msingi wa kuheshimiana
Sep 18, 2018 10:12Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za Afrika daima umekuwa ukiheshimu mamlaka ya kitaifa ya kila nchi na kutilia mkazo suala la ustawi na ushirikiano.
-
Sisitizo la IAEA la kutekeza Iran makubaliano ya nyuklia; na njama mpya za Donald Trump dhidi ya JCPOA
Sep 18, 2018 07:06Makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) yalitiwa saini Julai 2015 mjini Vienna Austria baina ya Iran na kundi la 5+1, linaloundwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Russia pamoja na Ujerumani na kuanza kutekelezwa Januari 2016.
-
Yukiya Amano asisitiza tena kwamba, Iran imetekeleza ahadi zake kuhusu JCPOA
Sep 17, 2018 11:12Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, Iran imekuwa ikitekeleza ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Qassemi: Madola huru yasimame kukabiliana na saiasa za kibeberu za Marekani
Sep 17, 2018 10:55Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kikao cha pande tatu cha Iran, Afghanistan na India kuhusiana na kuimarisha ushirikiano wa kieneo kilikuwa na mafanikio.
-
Salehi katika kikao cha IAEA mjini Vienna; sisitizo la majukumu na matarajio ya Iran kutoka kwa wakala huo
Sep 17, 2018 05:53Kikao cha 62 cha kila mwaka cha Wakala wa Kimataifa ya Nishati ya Atomiki IAEA kimeanza leo huko Vienna Austria.
-
Zarif ailaani Twitter kwa kutengeneza robot za kusajili watumiaji hewa ili kuipiga vita Iran
Sep 16, 2018 21:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kitendo cha mtandao wa kijamii wa Twitter kufunga hesabu za watumiaji wa kweli wa Kiirani katika mtandao huo na badala yake kutengeza roboti ambazo zinaendesha kampeni ya kuipindua Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.