-
Esper akadhibisha madai ya Trump kuhusu sababu za mauaji ya Jenerali Soleimani, asema hayana msingi
Jan 13, 2020 09:27Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper, amekadhibisha madai yaliyotolewa na Rais wa nchi hiyo Donald Trump kwamba Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa akipanga mashambulizi dhidi ya balozi nne za Marekani.
-
Trump na madai ya kizandiki ya kuwaunga mkono wananchi wa Iran
Jan 13, 2020 04:27Ijapokuwa tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipopata ushindi mwaka 1979 Marekani siku zote imekuwa ikiamiliana kiuadui na kiuhasama na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini Donald Trump, rais afriti aliyeko madarakani hivi sasa nchini humo, yeye ametia fora na kufurutu mpaka, kwa uadui ambao haujawahi kushuhudiwa, anaoifanyia Iran na wananchi wake.
-
Scott Ritter: Trump amelegeza msimamo kwa kuogopa jibu kali la Iran
Jan 11, 2020 01:21Scott Ritter, aliyewahi kuwa mkaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani amelegeza msimamo na kuachana na vitisho vyake alivyovitoa hapo kabla dhidi ya Iran kutokana na kuhofia jibu kali la Tehran.
-
Jenerali wa Marekani: Iran ina mbinu nyingi na hatari sana za kupambana na Marekani
Jan 04, 2020 13:35Barry McCaffrey, Jenerali wa Zamani wa Jeshi la Marekani amekiri kwamba Wairan wana mbinu nyingi na hatari sana za kijeshi kwa ajili ya kupambana na Marekani.
-
Marekani yaizuia Korea Kusini kutuma vifaa vyake vya kitiba nchini Iran
Dec 14, 2019 21:43Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imezungumzia upinzani wa Marekani kuhusiana na kutumwa bidhaa za kibinaadamu kama vile madawa, chakula na vifaa vya tiba kwenda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Russia: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimefeli
Nov 08, 2019 04:32Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina natija yoyote na vimefeli.
-
Trump na ahadi zake bandia za kuiondolea Iran vikwazo baada ya kufanyika mazungumzo
Sep 30, 2019 08:36Baada ya kuiondoa nchi yake kwenye mapatano ya nyuklia mwezi Mei mwaka jana na kisha kuiwekea vikwazo vikali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika miezi ya hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani ameonyesha hamu kubwa ya kutaka kufanya mazungumzo na Iran ambapo baada ya kufanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kulienea fununu za uwezekano wa kukutana marais wa Iran na Marekani kando ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Trump aagiza kuzidishwa ugaidi wa kiuchumi dhidi ya Iran
Sep 19, 2019 02:37Rais wa Marekani amemuagiza Waziri wa Fedha wa nchi hiyo kuweiwekea Iran vikwazo vikuu kufuatia kushindwa siasa za mashinikizo ya juu zaidi za Marekani dhidi ya nchi hii.
-
Ukosoaji wa Russia kwa nafasi haribifu ya Magharibi katika Ghuba ya Uajemi
Sep 10, 2019 22:01Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kuiondoa nchi hiyo katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mnamo tarehe 8 Mei mwaka uliopita, alianza kutekeleza mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran.
-
Mtazamo unaogongana wa Ulaya kuhusiana na JCPOA
Sep 10, 2019 02:44Licha ya kuwa Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya ( Ujerumani, Ufaransa na Uingrereza) zikiwa wanachama wa kundi la 4+1 zimekuwa zikisisitiza mara kwa mara udharura wa kulindwa mapatano ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), lakini hazijaweza kuwasilisha rekodi nzuri ya utendaji wao katika uwanja huo.