Marekani yaondoa madai ya kurejeshwa vikwazo vya UN dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i67028-marekani_yaondoa_madai_ya_kurejeshwa_vikwazo_vya_un_dhidi_ya_iran
Mwakilishi wa muda wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo na kuondoa madai ya serikali iliyotangulia ya nchi hiyo kuhusu kurejejeshwa vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 19, 2021 04:21 UTC
  • Marekani yaondoa madai ya kurejeshwa vikwazo vya UN dhidi ya Iran

Mwakilishi wa muda wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo na kuondoa madai ya serikali iliyotangulia ya nchi hiyo kuhusu kurejejeshwa vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.

Shirika la habari la Reuters limenukuu barua ya Richard Mills kwa Baraza la Usalama na kuandika: Marekani imeondoa madai ya serikali ya Donald Trump kuhusu kurejeshwa vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran. 

Serikali ya zamani ya Marekani chini ya uongozi wa Rais Donald Trump mwezi Agosti mwaka jana baada ya kushindwa kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran ilianzisha harakati zilizofeli kwa ajili ya kuirejeshea Iran vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Kurudi nyuma huko kwa Marekani kunajiri katika hali ambayo serikali mpya ya sasa ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Rais Joe Biden imekiri kufeli sera za Trump mkabala na Iran na kueleza kuwa ina lengo la kurejea katika mapatano ya JCPOA yaliyopasishwa na Baraza la Usalama kwa kuzingatia kujitoa Marekani kwa upande mmoja ndani ya mapatano hayo; hatua iliyopelekea kutengwa Marekani kimataifa. 

Rais Joe Biden wa Marekani 

Pamoja na hayo, viongozi wa serikali ya Biden siku kadhaa zilizopita walieleza kuwa, watarejea katika mapatano ya JCPOA baada ya Iran kuachana na eti hatua za ulipizaji kisasi. Viongozi wa Marekani wametamka hayo huku Washington ikiwa ndio iliyokiuka mapatano hayo ya nyuklia na kisha kujitoa kwa upande mmoja.