-
Iran: Mkwamo wa sasa wa JCPOA ni matunda ya sera ghalati za Marekani
Mar 01, 2023 07:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameikosoa na kuilaumu Marekani kwa kukwamisha mazungumzo ya kujaribu kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ya mwaka 2015.
-
"Uzoefu wa JCPOA umeipa Iran funzo la kutowategemea maajinabi"
Feb 05, 2023 10:49Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema Jamhuri ya Kiislamu imejifunza kutowategemea maajinabi kutokana na uzoefu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Muelekeo wa kiundumakuwili na wenye mgongano wa Marekani kuhusiana na JCPOA
Jan 11, 2023 09:18Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price amesema, hatua ya upande mmoja iliyochukuliwa na serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump ya kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni kosa kubwa zaidi la kistratejia lililofanywa katika miaka ya karibuni kwa upande wa sera za nje za Washington.
-
China: Mazungumzo ya JCPOA yapo katika marhala ya mwisho
Dec 27, 2022 07:26China imesema mazungumzo ya kujaribu kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yapo katika hatua ya mwisho, na kusisitiza kwamba fursa ya kufufua mapatano hayo ya kimataifa ingalipo.
-
Mazungumzo ya Josep Borrell na Amir-Abdollahian nchini Jordan; msimamo baridi wa Umoja wa Ulaya
Dec 21, 2022 02:16Jumanne ya jana tarehe 20 Disemba, Waziri wa Mashauri ya Kiigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya pambizoni mwa mkutano wa Baghdad-2 uliofanyika katika mji mkuu wa Jordan, Amman.
-
Iran: Marekani ikhitari diplomasia badala ya mashinikizo na vitisho
Dec 20, 2022 07:48Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema iwapo Marekani inataka kweli kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, haina chaguo jingine isipokuwa kukhitari njia ya diplomasia badala ya mashinikizo, vitisho na makabiliano.
-
Njama na hila za adui wa taifa la Iran za kulazimisha JCPOA 2 na JCPOA 3
Nov 27, 2022 12:58Baada ya Iran na nchi zilizounda kundi la 5+1 kufikia mwafaka Julai 2015 juu ya kadhia ya nyuklia ya Iran na kusaini Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, kwa kifupi JCPOA, nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani, -iwe ni baada ya kuanza kutekelezwa JCPOA mnamo mwaka 2016 au baada ya kujitoa Marekani kwenye makubaliano hayo Mei 2018, na hata katika kipindi cha sasa kufuatia duru kadhaa za mazungumzo ya Vienna ya uondoaji vikwazo vya kidhalimu-
-
Iran yaitaka Marekani iache unafiki katika mazungumzo ya JCPOA
Nov 17, 2022 07:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani ipo mbioni kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, na kwa msingi huo amewaasa viongozi wa nchi hiyo na timu ya wapatanishi wa Washington katika mazungumzo hayo kuweka pembeni unafiki.
-
Kukiri Marekani kuwa inahusika katika kuchochea ghasia na machafuko nchini Iran
Oct 15, 2022 03:40Ned Price, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, amekiri kwamba utawala wa Joe Biden sasa umejikita kwenye machafuko na ghasia nchini Iran huku akiiishutumu Tehran kuwa haiko tayari kufikia muafaka kuhusu kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Mbali na kukiri huko, imekuwa ikifahamika wazi kimataifa kuwa Marekani inaingilia masuala ya ndani ya Iran.
-
Abdollahian: Hatua za kuondolewa Iran vikwazo zipo katika mkondo sahihi
Oct 04, 2022 03:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema mazungumzo ya uondoaji vikwazo haramu ilivyowekewa Iran yanaendelea vizuri, na kwamba hatua za kuondolewa vikwazo hivyo zipo katika mkondo sahihi.