-
Larijani: Marekani ndiye mchochezi mkuu wa uhasama kati ya Iran na Saudia
Oct 16, 2019 01:06Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haina tatizo lolote wala haipingi mpango wowote wa kupatiwa ufumbuzi mikwaruzano na uhasama uliopo kati yake na Saudi Arabia, lakini Marekani ndiyo kizingiti kikuu katika kuafikiwa jambo hilo.
-
Spika wa Bunge la Iran aghairisha safari yake ya Uturuki baada ya nchi hiyo kuivamia kijeshi Syria
Oct 10, 2019 04:21Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameghairisha safari aliyokuwa amepanga kufanya nchini Uturuki kufuatia hatua ya nchi hiyo ya kuivamia kijeshi ardhi ya Syria.
-
Mkutano wa Tatu wa Mshikamamo na Vijana wa Palestina wafanyika Tehran
Oct 03, 2019 10:11Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Mshikamano na Watoto na Vijana wa Palestina kwa ajili ya kumkumbuka shahidi Muhammad al Durrah umefanyika hapa Tehran.
-
Larijani: Trump anafananisha medani ya siasa na ukumbi wa michezo ya kuigiza
Aug 20, 2019 22:45Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amekosea kufananisha medani ya siasa za uwanja wa michezo ya kuigiza na hatua hii inatoa pigo kwa hadhi ya taifa la Marekani.
-
Video inayowaonesha wanajeshi wa SEPAH wa Iran wakiionya manuwari ya kivita vya Uingereza isiingilie operesheni ya kuzuia meli ya mafuta ya nchi hiyo
Jul 29, 2019 16:18Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesambaza mkanda wa video na sauti wakati jeshi hilo lilipotoa onyo kwa Manuwari ya Kifalme wa Uingereza kwamba ikae mbali na isiingilie operesheni ya kusimamishwa meli ya mafuta iliyokuwa inapeperushwa bendera ya Uingereza katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Spika Larijani: Mkakati wa Iran ni kuinua kiwango cha usalama Mashariki ya Kati
Jul 28, 2019 23:52Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya stratijia ya Tehran ya kuinua kiwango cha usalama katika Mashariki ya Kati na kusema kwamba, usalama wa eneo hili unaweza kuletwa na nchi husika za eneo hili na si vinginevyo.
-
Spika wa Bunge la Iran: Sera za Saudia na Imarati zitawadhuru siku za usoni
Jun 02, 2019 10:55Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema sera za Saudi Arabia na Imarati (UAE) zitawadhuru katika siku za usoni.
-
Spika wa Bunge la Iran akosoa njama za Wamagharibi dhidi ya Wapalestina
May 26, 2019 23:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amekosoa vikali njama za nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zilizopewa jina la 'Muamala wa Karne' dhidi ya Wapalestina, huku akitoa mwito wa mahudhurio makubwa katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
-
Larijani: Wamarekani wafahamu kuwa Iran ni mshindani mgumu kwao
Apr 29, 2019 05:46Spika wa Bunge la Iran, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Ali Larijani amesema Wairani kamwe hawatasalimu amri mbele ya wanaotumia mabavu na kuongeza kuwa: "Wakuu wa Marekani wanapaswa kufahamu kuwa, Iran ni mshindani mgumu kwao."
-
Larijani: Nchi za Kiislamu zimeitelekeza Palestina
Apr 08, 2019 03:28Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Ali Larijani ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya nchi za Kiislamu ya kuitelekeza na kuiweka pembeni kadhia muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa, ambayo ni Palestina.