Oct 03, 2019 13:41 UTC
  • Mkutano wa Tatu wa Mshikamamo na Vijana wa Palestina wafanyika Tehran

Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Mshikamano na Watoto na Vijana wa Palestina kwa ajili ya kumkumbuka shahidi Muhammad al Durrah umefanyika hapa Tehran.

Mkutano huo wa kimataifa uliofanyika leo hapa Tehran kwa lengo la kuunga mkono mapambano ya wananchi wa Palestina umehudhuriwa na maafisa wa serikali, jeshi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa na shaksiya wa kiutamaduni, kisiasa, kidini, wanafunzi na vijana kutoka nchi mbalimbali duniani. Ujumbe wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ulisomwa kwenye mkutano huo uliohudhuriwa pia na wanafunzi kutoka Iran, Palestina, Yemen, Syria, Lebanon, Iraq, Bosnia Herzegovina na nchi nyingine kadhaa. 

Katika sehemu moja ya ujumbe wake Spika wa Bunge la Iran Dakta  Ali Larijani amepongeza maadhimisho ya kumkumbuka Shahidi Muhammad al Durrah na kueleza kuwa: Mtoto huyo wa Kipalestina aliuawa kwa kupigwa risasi moja kwa moja na adui Mzayuni akiwa amejibanza ubavuni mwa baba yake mbele ya macho ya kanali na televisheni na vyombo vya habari, lakini taasisi za kimataifa zilimtetea na kumkingia kifua muuaji badala ya kumtetea aliyedhulumiwa. 

Shahidi Muhammad al Durrah alieuliwa shahidi kwa kupigwa risasi kadhaa na mwanajeshi wa Israel.
 

Muhammad al Durrah mtoto wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 12 aliuawa shahidi mwaka 2000 baada ya kupigwa risasi kadhaa na mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel akiwa amejificha ubavuni mwa baba yake, huku baba yake, wananchi na vyombo vya habari vikishuhudia jinai hiyo. 

Wizara ya Habari ya Palestina imetangaza kuwa tangu mwaka 2000 mwanzoni mwa mapambano ya Intifadha ya Pili hadi kufikia mwezi Februari mwaka 2017, watoto wa Kipalestina 2,069 wameuawa kwenye mashambulizi ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu. 

Tags