-
Radiamali ya Sayyid Hassan Nasrullah kuhusu kadhia ya Amer Al-Fakhoury
Mar 22, 2020 04:49Kuachiliwa huru na kutoroshwa Amer Al-Fakhoury, kibaraka mwenye uraiapacha wa Lebanon na Marekani, ilikuwa ndio maudhui kuu ya hotuba aliyotoa Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon usiku wa kuamkia jana.
-
Uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya Lebanon na kuendelea mwenendo ulio dhidi ya Hizbullah
Mar 15, 2020 05:56Katika kikao cha Ijumaa iliyopita pamoja na Hassan Diab, Waziri Mkuu wa Lebanon, Dorothy Shea, balozi mpya wa Marekani nchini Lebanon sambamba na kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu, alisema kuwa mazingira ya msaada wa Washington kwa ajili ya kuushinda mzozo wa kiuchumi wa taifa hilo, unategemea kutengana serikali ya Beirut na Harakati ya Muqawama ya Hizbullah.
-
Lebanon yachukua uamuzi wa kuanza kuchimba mafuta eneo inalozozania na Israel
Feb 27, 2020 21:47Rais Michel Aoun wa Lebanon ametangaza kuwa nchi yake itaanzisha operesheni ya kuchimba mafuta katika eneo inalozozania na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Askofu wa Kanisa Katoliki Lebanon: Mpango wa Muamala wa Karne ni namna fulani ya kutangaza vita
Feb 19, 2020 08:11Kiongozi wa Kanisa Katoliki kusini mwa Lebanon amesema kuwa, mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne unakinzana wazi kabisa na amani na kuishi pamoja na kimsingi ni namna fulani ya kutangaza vita.
-
Spika wa Iran akutana na Rais wa Lebanon na Sayyid Nasrullah
Feb 18, 2020 04:22Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Michel Aoun wa Lebanon, Spika wa Bunge la nchi hiyo ya Kiarabu, Nabih Berri na Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah mjini Beirut.
-
Kuundwa serikali mpya ya Lebanon; mafanikio na changamoto
Feb 13, 2020 04:39Bunge la Lebanon siku ya Jumanne liliidhinisha baraza jipya la mawaziri la nchi hiyo ambalo lilipendekezwa na Waziri Mkuu Hassan Diab. Baraza hilo lilipitishwa kwa kura 63 za 'ndio' na 20 za 'la' huku mbunge mmoja akijizuia kupiga kura katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wabunge 84 kati ya wabunge wote 128 wa Bunge la Lebanon.
-
Hizbullah ya Lebanon: Tutaiunga mkono serikali mpya
Feb 08, 2020 04:29Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbulla ya Lebanon amesema kuwa harakati hiyo itaonyesha imani yake kwa serikali mpya ya nchi hiyo kwa kuwa ina shakhsia wanaofaa.
-
Hizbullah: Marekani ndiyo sababu ya matatizo yote ya Lebanon
Jan 26, 2020 09:26Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ndiyo chimbuko la matatizo yote yanayoikabili Lebanon.
-
"ISIS walitaka kushambulia ubalozi wa Marekani Lebanon na kuisingizia Hizbullah"
Jan 24, 2020 02:45Gazeti la al Jamhuriyyah la Lebanon limefichua kuwa, genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lilikuwa limepanga njama za kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Beirut ili kuibebesha lawama harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Hizbullah hasa baada ya Marekani kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Jasusi mmoja wa Marekani atiwa mbaroni mjini Beirut, Lebanon
Jan 20, 2020 09:44Maafisa usalama wa Lebanon wamemtia mbaroni mwandishi mmoja wa habari wa Kimarekani katika maandamano ya wananchi mjini Beirut kwa tuhuma za kuufanyia ujasusi utawala haramu wa Kizayuni.