Lebanon yachukua uamuzi wa kuanza kuchimba mafuta eneo inalozozania na Israel
Rais Michel Aoun wa Lebanon ametangaza kuwa nchi yake itaanzisha operesheni ya kuchimba mafuta katika eneo inalozozania na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Rais Aoun amesema kuwa sasa Lebanon itajiunga na nchi nyingine zinazozalisha mafuta na kwamba hatua hiyo itakuwa ya kihistoria kwa nchi hiyo. Akibainisha kwamba matatizo ya ndani na ya kisiasa nchini Lebanon ndio yalizuia operesheni ya kugundua na kuchimba mafuta mwaka 2013, amebainisha kwamba uchimbaji huo wa mafuta unaweza kugeuza uchumi wa nchi hiyo na kuufanya kuwa sawa na wa nchi nyingine yoyote inayozalisha mafuta.
Inafaa kuashiria kuwa Lebanon na utawala haramu wa Kizayuni zinatofautiana kuhusu uainishaji mipaka katika bahari ya Mediterrania ambapo mwaka 2018 tofauti hizo zilishtadi zaidi juu ya eneo lenye mafuta la Namba Tisa. Kwa kuzingatia kuwa eneo linalozozaniwa katika bahari ya Mediterrania ni lenye nishati ya mafuta na gesi, hivyo utawala bandia wa Kizayuni na kwa mara kadhaa umetoa vitisho dhidi ya serikali ya Beirut kwamba utahakikisha unaizuia nchi hiyo ya Kiarabu kuweza kunufaika na nishati hizo.