-
HRW: Shambulizi la 'drone' ya Imarati liliua raia 8 Tripoli, Libya
Apr 30, 2020 03:38Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema shambulizi la ndege isiyo na rubani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) dhidi ya mji mkuu wa Libya, Tripoli mwishoni mwa mwaka jana liliua na kujeruhi raia wasio na hatia.
-
Russia: Hatulitambui tangazo la serikali ya Haftar nchini Libya
Apr 29, 2020 22:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, serikali ya Moscow haikubali utawala wa kujitwika wa kiongozi wa wanamgambo wanaojiita 'Jeshi la Kitaifa la Libya' nchini humo.
-
Msimamo wa Umoja wa Mataifa wa kukataa kuitambua serikali ya Libya aliyojitangazia Haftar
Apr 29, 2020 22:06Kufuatia hatua ya Jenerali muasi Khalifa Haftar ya kukiuka mapatano ya Skhirat na kujitangazia serikali nchini Libya, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa unaitambua rasmi tu Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa (GNA) yenye makao yake Tripoli.
-
Makabila ya Muammar al-Gaddafi na Aguila Saleh yapinga tangazo la Haftar kuwa yeye ndiye mtawala wa Libya
Apr 29, 2020 12:09Duru za kieneo pamoja na bunge lenye makao yake mjini Tobruk zimemwandikia barua jenerali muasi, Khalifa Haftar, zikitangaza upinzani wao kwa hatua yake ya kujitangaza kuwa yeye ndiye mtawala wa Libya.
-
Umoja wa Mataifa wakataa kuitambua serikali ya Libya aliyojiundia Haftar
Apr 28, 2020 22:32Umoja wa Mataifa umetangaza msimamo wake kuhusu hatua aliyochukua jenerali muasi wa Libya Khalifa Haftar ya kujitangaza mtawala wa nchi hiyo na kusisitiza kuwa, unayoitambua umoja huo ni Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa (GNA) pekee na si mtu mwingine yeyote.
-
Kubatilisha Khalifa Haftar makubaliano ya Skhirat na kujitangaza kuwa kiongozi wa Libya
Apr 28, 2020 20:18Katika hali ambayo mapigano baina ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa Libya na wanamgambo watiifu kwa Khalifa Hatar yangali yanaendelea, jenerali huyo muasi amechukua hatua ya upande mmoja ya kuvunja makubaliano ya kisiasa ya Skhirat na kujitangaza kuwa kiongozi wa nchi hiyo.
-
Wanamgambo watiifu kwa Jenerali muasi Haftar washambulia msikiti katika mji mkuu wa Libya
Apr 27, 2020 03:22Kikosi cha mizinga cha wanamgambo wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar, kimeshambulia msikiti katika mji mkuu wa Libya, Tripoli pamoja na maeneo ya makazi ya raia kandokando ya mji huo.
-
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa Libya yapinga mpango wa EU wa kuzuia kuingizwa silaha nchini humo
Apr 25, 2020 08:43Vita vya ndani nchini Libya vilivyoanza baada ya kung'olewa madarakati dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi vimeshika mwelekeo unaotia wasiwasi mkubwa zaidi tangu Aprili mwaka jana 2019 kufuatilia mashambulizi ya wapiganaji wa linalojiita jeshi la taifa la Libya chini ya uongozi wa Khalifa Haftar, lengo likiwa ni kuudhibiti mji mkuu, Tripoli na kuing'oa madarakani Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa.
-
Ripoti: UAE inashirikiana na Sudan kuunga mkono waasi wa Haftar nchini Libya
Apr 25, 2020 06:34Gazeti moja la Libya limefichua kuhusu mapatano mapya ya Sudan na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa lengo la kumuunga mkono kinara wa waasi Libya, Jenerali Khalifa Haftar.
-
Libya: Watawala wa Imarati ndio wanaosababisha maafa nchini mwetu
Apr 23, 2020 07:08Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa ya Libya amesema kuwa, watawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ndio wanaosababisha maafa nchini Libya kutokana na wanamgambo wake walioko chini ya jenerali muasi Khalifa Haftar kutumia gesi za sumu katika mashambulizi yao.