-
Al Sisi: Misri inaunga mkono ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Libya
Dec 26, 2019 22:53Rais wa Misri amesema kuwa nchi yake inataka kulinda ardhi kamili ya Libya na inakaribisha utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo.
-
Rais Erdogan wa Uturuki afanya safari ya ghafla Tunisia kujadili usitishaji vita nchini Libya
Dec 26, 2019 04:22Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki jana alifanya safari ya ghafla nchini Tunisia kujadili namna ya kushirikiana na nchi hiyo ili kutafuta uwezekano wa kufanikisha usitishaji vita katika nchi jirani ya Libya, ambapo Ankara ni muungaji mkono wa serikali ya nchi hiyo inayotambuliwa rasmi kimataifa.
-
Mgogoro wa Libya na uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo
Dec 24, 2019 00:56Tukio la kutiwa saini makubaliano ya kijeshi na kiusalama na ushirikiano wa baharini kati ya Uturuki na serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya limezikasirisha nchi kadhaa za kikanda na nje ya kanda hiyo.
-
Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya yapinga mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki na Haftar
Dec 23, 2019 10:16Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amelaani safari ya waziri mwenzake wa Ugiriki huko mashariki mwa Libya na mazungumzo aliyofanya na Khalifa Haftar na viongozi wa serikali inayomuunga mkono.
-
Uturuki yatangaza kuwa tayari kutuma wanajeshi wake Libya kuisaidia serikali ya Sarraj
Dec 23, 2019 03:44Makamu wa Rais wa Uturuki Fuat Oktay ametangaza kuwa, 'iwapo serikali ya muafaka wa kitaifa Libya itawasilisha ombi rasmi, Uturuki iko tayari kutuma wanajeshi wake katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.
-
Fayez al Sarraj: Mashambulizi ya droni za Imarati hayatasalia bila jibu
Dec 22, 2019 03:23Fayez al Sarraj Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya jana usiku alisema kuwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) za Imarati katika maeneo ya Zliten na Msalata kaskazini mwa nchi hiyo ni hatua ya kihalifu ambayo haitasalia bila ya jibu.
-
Libya: Misri, Saudia, Imarati zinavunja azimio la Baraza la Usalama
Dec 20, 2019 23:34Mwakilishi wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, nchi za Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinavunja azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa uungaji mkono wao kwa jenerali muasi, Khalifa Haftar.
-
Rais Putin wa Russia ataka kuhitimishwa mgogoro wa Libya
Dec 19, 2019 09:25Rais Vladimir Putin wa Russia amesema angependa kuona mgogoro wa Libya unapatiwa ufumbuzi na mazungumzo baina ya pande mbili hasimu katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika yanaanza.
-
Libya na Misri wazidi kuzozana baada ya Cairo "kuidhalilisha" Tripoli
Dec 18, 2019 08:05Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya imekasirishwa mno na matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri na imetoa majibu makali dhidi ya Cairo ikisema huo ni udhalilishaji kwa taifa la Libya.
-
Mgogoro wa kidiplomasia, Libya yafunga ubalozi wake Misri
Dec 15, 2019 04:27Libya imetangaza habari ya kufunga ubalozi wake katika mji mkuu wa Misri Cairo, kutokana na kile kilichotajwa kuwa sababu za kiusalama.