Sep 11, 2016 06:07
Rais Barack Obama wa Marekani ameonesha kukasirishwa sana na hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya majaribio ya tano ya nyuklia, huku viongozi wa Pyongyang wakisema kuwa, wamefanya majaribio hayo ili kujibu siasa za kiuadui za Marekani na waitifaki wake dhidi ya Korea Kaskazini.