Iran yarusha kwa mafanikio kombora jipya zaidi la baharini la Cruz
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa kombora jipya zaidi la baharini la Iran kwa jina la "Nassir" limefanyiwa majaribio kwa mafanikio katika maneva ya jeshi la wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Brigedia Jenerali Hussein Dehqan Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema leo kuwa, kombora jipya zaidi la baharini la Iran la Cruz lililopewa jina la "Nassir" limerushwa kwa mafanikio katika maneva kubwa ya jeshi la wanamaji la Iran kwa jina la Velayati-95 yanayofanyika katika maji ya kusini mwa Iran pamoja na kufanyiwa pia majaribio makombora mengine yaliyotengenezwa humu nchini. Makombora hayo yanayoongozwa kwa mfumo wa laser yanayolenga nyambizi baharini kwa jina la Dehlaviyeh yamefanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika maneva hayo.
Maneva hiyo ya jeshi la wanamaji la Iran kwa jina la Velayati - 95 yalianza jana asubuhi katika eneo la ukubwa wa kilomita mraba milioni mbili kutoka lango la Hormoz, bahari ya Oman, eneo la kaskazini mwa bahari ya Hindi na lango la Babul Mandab. Admeri Habibullah Sayari Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran amesema maneva hayo yamefanyika lengo likiwa ni kulinda mipaka ya majini na kudumisha usalama katika eneo, kupambana na maharamia wa baharini, ugaidi na kutuma ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi za eneo.