Saudia yazidi kujipenyeza kijeshi Afrika, yaandaa luteka na Sudan
(last modified Mon, 27 Mar 2017 07:54:08 GMT )
Mar 27, 2017 07:54 UTC
  • Saudia yazidi kujipenyeza kijeshi Afrika, yaandaa luteka na Sudan

Katika hatua inayoonekana ni ya kujaribu kujienyeza zaidi kijeshi barani Afrika, majeshi ya Saudi Arabia na Sudan yanatazamiwa kufanya luteka ya pamoja wiki hii.

Salaheddin Abdul Khalid, Kaimu Mkuu wa Jeshi la Angani la Sudan amesema mazoezi hayo ya kijeshi yanatazamiwa kuanza Machi 29 na kumalizika Aprili 12, katika eneo la Meroe, kaskazini mwa mji mkuu Khartoum.

Amesema katika maneva hayo ya kijeshi, aina 24 za ndege za kivita zikiwemo za MiG-29 na Sukhoi zitatumika. Aidha ndege za kivita za Saudia aina ya F-15 na Eurofighter Typhoons zitashirikishwa katika luteka hiyo.

Ndege za kijeshi katika katika luteka

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Khartoum imekuwa ikijikurubisha kwa Saudia na kufuata kibubusa sera za Riyadh kwa lengo la kutaka kupewa misaada mbalimbali.

Hivi karibuni, Abayomi Azikiwe, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwandishi wa habari wa kiafrika alisema kuwa, uamuzi wa serikali ya Marekani wa kuiondolea Sudan baadhi ya vikwazo ilivyokuwa imeiwekea ni malipo ya Khartoum baada ya kubadili msimamo wake kuhusu nchi za Magharibi na kuimarisha uhusiano wake na Saudi Arabia. 

Tags