-
Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru Nigeria
Apr 08, 2018 09:19Watu wa Nigeria wameendeleza maandamano yao ya kulaani hatua ya serikali kuendelea kumshikilia kinyume cha sheria kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky huku wakitaka aachiliwe huru mara moja.
-
Vikosi vya usalama Bahrain vyawashambulia waandamanaji
Apr 07, 2018 03:24Maafisa usalama wa Bahrain wamewashambulia wananchi waliokuwa wamemininika mabarabarani kushiriki maandamano ya kupinga kufanyika nchini humo mashindano ya magari ya Langalanga maarufu kama Formula 1.
-
Wapalestina waandamana katika Ijumaa ya pili ya maandamano ya "Haki ya Kurejea"
Apr 06, 2018 09:34Maelfu ya Wapalestina wamejitokeza leo na kuandamana huko Gaza Palestina katika Ijumaa ya pili ya maandamano ya "Haki ya Kurejea".
-
Waingereza waandamana kuonyesha mshikamano wao na Wapalestina
Apr 01, 2018 12:51Wananchi na makundi ya kiraia katika mji wa London nchini Uingereza wamefanya maandamano wakitangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kulaani jinai wanazofanyiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wapalestina 8 wauawa shahidi na jeshi la Israel katika maandamano ya Siku ya Ardhi
Mar 30, 2018 11:24Kwa akali Wapalestina wanane wameuawa shahidi na wanajeshi katili wa Israel katika maandamano ya Siku ya Ardhi, ya kulaani hatua ya utawala huo ghasibu ya kupora ardhi zao, yaliyofanyika leo karibu na uzio wa kibaguzi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Waguinea waandamana kupinga ukatili wa polisi
Mar 30, 2018 03:22Wananchi wa Guinea wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry wakipinga ukatili wa polisi dhidi ya wafuasi wa kambi ya upinzani na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya polisi waliohusika na mauaji ya raia.
-
Wananchi Ghana wapinga mkataba wa kijeshi na Marekani
Mar 29, 2018 01:56Maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Ghana, Accra siku ya Jumatano kupinga mkataba tata wa kijeshi baina ya nchi yao na Marekani.
-
Bin Salman akaribishwa Marekani kwa maandamano ya kulaani mauaji ya watoto Yemen
Mar 20, 2018 12:20Maelfu ya wanaharakati wamefanya maandamano nje ya jengo la Capitol Hill lenye mabunge ya Marekani katika jiji la Washington, kulaani mauaji ya watoto wadogo wasio na hatia nchini Yemen yanayofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia.
-
Wanachuo wanaosomea utabibu wafanya maandamano nchini Tunisia
Mar 13, 2018 04:31Wanafunzi wanaosomea taaluma ya udakitari nchini Tunisia wamefanya maandamano nje ya ofisi ya Wizara ya Afya wakishinikiza kutekelezewa matakwa yao.
-
Maelfu ya wahajiri wa Kiafrika waandamana Italia kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo
Mar 11, 2018 03:47Maelfu ya wahajiri wa Kiafrika pamoja na raia wengi wa Italia wameandamana katika mji wa Florence kaskazini mwa Italia kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini humo.