Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42814-maandamano_ya_kutaka_sheikh_zakzaky_aachiliwe_huru_nigeria
Watu wa Nigeria wameendeleza maandamano yao ya kulaani hatua ya serikali kuendelea kumshikilia kinyume cha sheria kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky huku wakitaka aachiliwe huru mara moja.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 08, 2018 09:19 UTC
  • Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru Nigeria

Watu wa Nigeria wameendeleza maandamano yao ya kulaani hatua ya serikali kuendelea kumshikilia kinyume cha sheria kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky huku wakitaka aachiliwe huru mara moja.

Kwa mujibu wa taarifa, maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja huku waandamanaji wakiwa wamebeba mabango ya kulaani serikali na jeshi la nchi hiyo kwa kuendelea kumshikilia Sheikh Zakzaky.

Washiriki wa maandamano hayo wamesisitiza kuendeleza kujitokeza mitaani hadi pale serikali itakaposikiliza takwa lao na kumuachilia huru Sheikh Zakzaky.

Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake walitekwa nyara na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 wakati askari walipovamia kituo chake cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashtaka.

Wanigeria wakiwa katika maandamano ya amani ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

Uvamizi huo ulijiri baada ya Jeshi la Nigeria kudai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua mkuu wa jeshi hilo, madai ambayo yalikanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.

Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo huku Sheikh Zakzaky, ambaye hali yake ya kiafya si nzuri, akiendelea kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtaka.