Waguinea waandamana kupinga ukatili wa polisi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i42396-waguinea_waandamana_kupinga_ukatili_wa_polisi
Wananchi wa Guinea wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry wakipinga ukatili wa polisi dhidi ya wafuasi wa kambi ya upinzani na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya polisi waliohusika na mauaji ya raia.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Mar 30, 2018 03:22 UTC
  • Waguinea waandamana kupinga ukatili wa polisi

Wananchi wa Guinea wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry wakipinga ukatili wa polisi dhidi ya wafuasi wa kambi ya upinzani na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya polisi waliohusika na mauaji ya raia.

Mamia ya wanawake walioshiriki katika maandamano hayo walikuwa wamebeba picha za watu waliouawa na jeshi la polisi katika maandamano ya wapinzani. 

Wafuasi wa kambi ya upinzani nchini Guinea Conakry wamekuwa wakifanya maandamano ya amani wakipinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo Februari mwaka huu. Raia kadhaa wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa na polisi katika maandamano hayo. 

Wapinzani wa Rais Alpha Condé wa Guinea wanasema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu. 

Uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 4 Februari nchini Guinea ulikuwa wa kwanza wa aina yake tangu ulipokomeshwa utawala wa kijeshi nchini humo na kufuatia miaka nane ya kucheleweshwa zoezi hilo kutokana na ukosefu wa fedha, mivutano ya kisiasa na mgogoro wa Ebola 2013-16.