-
Indhari na hatua mpya kuhusu vita vya ushuru vya Trump
Apr 27, 2025 02:26Indhari na radiamali mpya zimetolewa ndani ya Marekani na kimataifa kutokana na kuendelea vita vya ushuru vya Rais Donald Trump na madai yake katika uwanja huo.
-
National Interest: Mji wa makombora wa Iran unaonyesha nguvu ya nchi hiyo
Apr 01, 2025 02:46Gazeti la Marekani la National Interest limeuchambua mji mpya wa makombora wa Iran na kusisitiza kwamba, kufichuliwa mji huo huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika Bahari Nyekundu na Asia Magharibi, ni ujumbe kwa Marekani na maadui wa Iran.National Interest imekiri katika ripoti yake kwamba hifadhi ya makombora ya Iran imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita.
-
Mwanamke anayechukia Waislamu apatikana na hatia ubadhirifu Ufaransa
Apr 01, 2025 02:40Mahakama moja nchini Ufaransa jana Jumatatu ilimpata na hatia ya ubadhirifu, Marine Le Pen, aliyekuwa mgombea urais wa Ufaransa kwa mihula miwili na kiongozi wa chama cha National Rally (RN) chenye chuki dhidi ya Waislamu. Hukumu hiyo itaathiri mustakabali wake wa kisiasa, hasa kugombea katika uchaguzi wa rais wa Ufaransa wa 2027.
-
Netanyahu anasa kwenye dema la Mahakama ya Uhalifu
Jan 28, 2025 02:56Baada ya kusita kwa muda wa mwezi mmoja, hatimaye mahakama ya kesi za uhalifu ya Israel imeanza tena kusikiliza kesi za uhalifu za waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
-
Mahakama ya New York yamhukumu Trump katika kesi ya ufisadi
Jan 11, 2025 06:38Mahakama ya New York jana ilitoa hukumu yake dhidi ya rais mteule wa Marekani, Donald Trump katika kesi ya faili la ufisadi wa kingono.
-
Jaji: Hukumu dhidi ya Trump kutolewa kabla ya kuapishwa kwake
Jan 05, 2025 03:35Jaji wa New York ametangaza kuwa, hukumu dhidi ya Donald Trump Rais mteule wa Marekani itatolewa tarehe 10 ya mwezi huu wa Januari katika kesi yake ya fedha mjini New York siku chache kabla ya kuapishwa kuwa rais.
-
ICC: Mawasiliano na ufuatiliaji unaendelea kufanywa ili kuwatia nguvuni Netanyahu na Gallant
Dec 15, 2024 05:35Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imetangaza kuwa, mawasiliano na ufuatiliaji mkubwa unaendelea kufanywa ili kuweza kuwatia mbaroni waziri mkuu pamoja na waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Shirikisho la Wanahabari: Waandishi 104 wameuliwa 2024, zaidi ya nusu wameuawa Ghaza
Dec 10, 2024 11:26Shirikisho la Kimataifa la Wanahabari (IFJ) limetangaza leo kuwa 2024 umekuwa mwaka wa "mauti zaidi" kwa waandishi wa habari kutokana na waandishi 104 wa habari kuuawa duniani kote, huku zaidi ya nusu kati yao wakiuawa katika Ukanda wa Ghaza.
-
Watu 26 wahukumiwa kifo Kongo DR kwa 'jinai za kivita'
Aug 09, 2024 03:27Watu wasiopungua 26 wamehukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka matatu yaliyokuwa yakiwakabili.
-
Mahakama Iran: Sharti US iwape fidia wagonjwa wa kipepeo kutokana na vikwazo
Jul 12, 2024 03:04Mahakama moja nchini Iran imeiagiza Marekani kulipa takriban dola bilioni 7 kama fidia kwa waathiriwa wa ugonjwa wa ngozi wa Epidermolysis Bullosa (EB) nchini Iran.