-
Mahakama ya Juu ya Liberia yasimamisha duru ya pili ya uchaguzi wa rais
Nov 06, 2017 10:16Kwa mara nyingine tena Mahakama ya Juu ya Liberia imesimamisha kwa muda usiojulikana kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyotazamiwa kufanyika kesho Jumanne.
-
Mahakama ya Juu Iraq yapiga marufuku kujitenga eneo lolote nchini
Nov 06, 2017 10:13Mahakama ya Juu ya Federali ya Iraq imepiga marufuku mpango wowote wa kujitenga mkoa au eneo lolote la nchi hiyo, kufuatia mgogoro uliosababishwa na jaribio la kutaka kujitenga eneo la Kurdistan kinyume cha katiba.
-
Rais Mugabe ataka kurejeshwa hukumu ya kifo nchini Zimbabwe
Nov 02, 2017 04:46Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametoa mwito wa kurejeshwa hukumu ya kifo baada ya watu 50 kutuma maombi ya kujaza nafasi iliyo wazi ya mtu wa kutekeleza adhabu ya kunyongwa.
-
Mahakama Kuu ya Liberia yasimamisha duru ya pili ya uchaguzi wa rais
Nov 02, 2017 04:06Mahakama ya Juu nchini Liberia imesimamisha duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyotazamiwa kufanyika mapema wiki ijayo, kutokana na madai ya uchakachuaji na dosari chungu nzima katika uchaguzi wa Oktoba 10.
-
Mahakama ya Uhispania yatengua 'uhuru' wa Catalonia
Oct 31, 2017 10:08Mahakama ya Katiba nchini Uhispania imebatilisha azimio lililopasishwa na bunge la eneo la Catalonia la kutangaza uhuru wa eneo hilo Ijumaa iliyopita.
-
Mahakama ya Pakistan yaagiza kukamatwa Waziri Mkuu wa zamani
Oct 26, 2017 04:32Mahakama moja nchini Pakistan imetoa waranti wa kukamatwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Nawaz Sharif, baada ya kukosa kufika mahakamani kusikiliza kesi ya ufisadi inayomwandama.
-
Mashirika ya kutetea haki za binadamu Marekani yampeleka Trump kotini
Sep 30, 2017 04:40Mashirika ya kutetea haki za binadamu katika jimbo la Maryland nchini Marekani yameenda mahakamani kuushtaki utawala wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo juu ya marufuku mpya iliyo dhidi ya wahajiri.
-
Mahakama ya kimataifa Malaysi yatoa hukumu dhidi ya viongozi wauaji wa Myanmar
Sep 23, 2017 12:13Mahakama ya Kimataifa ya Kudumu ya Watu wa Malaysia imetoa hukumu dhidi ya serikali ya Myanmar kutokana na kutenda jinai za mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.
-
Mahakama ya Juu Kenya yatoa ufafanuzi wa kubatilisha uchaguzi wa urais
Sep 20, 2017 09:47Mahakama ya Juu nchini Kenya imesema haijuti kuchukua uamuzi wa kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8 mwaka huu, huku ikiilaumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kwa kuendesha zoezi hilo kinyume cha sheria.
-
Majaji wasitisha mgomo wa miezi minne nchini Sudan Kusini
Sep 10, 2017 03:12Majaji na mahakimu nchini Sudan Kusini wametangaza kusitisha mgomo wao wa miezi minne baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kuahidi kutimiza matakwa yao.