Mahakama ya Juu Iraq yapiga marufuku kujitenga eneo lolote nchini
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36206-mahakama_ya_juu_iraq_yapiga_marufuku_kujitenga_eneo_lolote_nchini
Mahakama ya Juu ya Federali ya Iraq imepiga marufuku mpango wowote wa kujitenga mkoa au eneo lolote la nchi hiyo, kufuatia mgogoro uliosababishwa na jaribio la kutaka kujitenga eneo la Kurdistan kinyume cha katiba.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 06, 2017 10:13 UTC
  • Mahakama ya Juu Iraq yapiga marufuku kujitenga eneo lolote nchini

Mahakama ya Juu ya Federali ya Iraq imepiga marufuku mpango wowote wa kujitenga mkoa au eneo lolote la nchi hiyo, kufuatia mgogoro uliosababishwa na jaribio la kutaka kujitenga eneo la Kurdistan kinyume cha katiba.

Mahakama hiyo imepasisha uamuzi huo leo Jumatatu baada ya serikali ya nchi hiyo kuiomba ichukue hatua ya kusimamisha 'kutafsiriwa kimakosa' Katiba ya nchi.

Aidha mahakama hiyo yenye mamlaka ya kusuluhisha mizozo kati ya serikali kuu ya Baghdad na maeneo yenye mamlaka ya ndani ya nchi hiyo imesema imechukua hatua hiyo kwa shabaha ya kulinda umoja wa wananchi wa Iraq.

Masou Barazani, aliyekuwa Rais wa Kurdistan ya Iraq

Mwezi uliopita, Rais wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Kurdistan (KRG) nchini Iraq Masoud Barzani alitangaza kujiuzulu baada ya kuitisha kura ya maoni mnamo Oktoba 25, licha ya pingamizi kutoka ndani na nje ya nchi.

Bunge la Iraq lilipinga kufanyika kura hiyo ya maoni ya kujitenga Kurdistan na maeneo mengine yote ya Iraq, likisisitiza kuwa zoezi hilo ni kinyume cha katiba.