-
Ripoti: Nchi 125 zawajibika kisheria kumkamata Netanyahu huku hati ya ICC ikimnyemelea Waziri Mkuu huyo wa Israel
Aug 27, 2026 04:20Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anakabiliwa na vizuizi vikali kimataifa vya kusafiri huku nchi 125 duniani zikiwajibika kisheria kwa kuwa wanachama katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kumtia mbaroni mtenda jinai huyo iwapo awasili katika nchi hizo.
-
ICC yalaani na kupinga vikali vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya maafisa wake
Aug 20, 2026 10:36Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, imelaani na kupinga vikali hatua ya serikali ya Marekani ya kumuwekea vikwazo Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Tomoko Akane kutoka Japan, na Wakili Mwandamizi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka, Abdoulaye Seye kutoka Senegal.
-
Chad kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, yasema inaziandama zaidi nchi za Afrika
Jul 28, 2026 03:52Chad imejiunga na orodha inayoongezeka ya nchi zilizoanza taratibu za kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ikisema inaziandama zaidi nchi za Afrika.
-
Mwendesha-mashtaka wa ICC Karim Khan aondolewa kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono
Jul 25, 2026 02:58Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) umepiga kura ya kumwondoa Mwendesha Mashtaka Karim Khan kufuatia madai ya utovu wa nidhamu wa kingono; timu yake ya wanasheria imethibitisha hayo, huku ikidokeza kuwa hatua hiyo ilikuwa ya "kisiasa".
-
Waghana waiomba ICC kuchunguza ukatili wa chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini
Jul 24, 2026 02:48Raia wawili wa Ghana wamewasilisha ombi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wakiitaka kufungua uchunguzi wa awali kuhusu vitendo vya ukatili vinavyowalenga wageni nchini Afrika Kusini, wakisema kwamba muundo, ukubwa na kukaririwa mashambulizi yanayowalenga wahamiaji vinaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
-
EU yaunga mkono ICC, yapinga kampeni ya Trump ya kuvunja mahakama ya uhalifu wa kivita
Jul 16, 2026 02:55Umoja wa Ulaya (EU) umesisitiza tena uungaji mkono wake kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ukipinga kampeni mpya ya utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump ya kudhoofisha mahakama hiyo yenye makao yake makuu The Hague nchini Uholanzi.
-
ICC 'yahofia' kuhusu kujiondoa kwa Mali, Burkina Faso na Niger
Jul 02, 2026 11:35Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeeleza wasiwasi wake kuhusu kujiondoa Mali, Burkina Faso na Niger kwenye mahakama hiyo, ikisema kunadhoofisha harakati za kimataifa za kutafuta haki.
-
ICC yamsimamisha Kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu wa kingono
Jun 09, 2026 09:48Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemsimamisha kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan, kwa madai ya utovu wa nidhamu wa kingono na msaidizi wake.
-
ICC: Vikwazo vya US ni 'hujuma' dhidi ya haki duniani
Dec 19, 2025 07:43Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imelaani vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya majaji wawili wa korti hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Mwendesha Mashtaka wa ICC aikosoa Marekani kwa kuwafananisha majaji wa mahakama hiyo na magaidi, walanguzi wa dawa za kulevya
Dec 06, 2025 10:27Naibu mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ameikosoa vikali serikali ya Marekani kwa kuwawekea vikwazo majaji wa mahakama hiyo ya kimataifa, hatua ambayo amesema inaakisi jinsi Washington inavyowalenga magaidi na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.