-
Raisi: Vikwazo vipya vinaonesha Iran ina haki ya kutoiamini Marekani
Jun 17, 2022 07:25Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Marekani kwa upande mmoja kudai kuwa ina nia ya kweli ya kufanya mazungumzo na Iran na wakati huohuo inatangaza vikwazo vipya dhidi ya taifa hili kwa upande mwingine, inaonesha wazi kuwa Tehran ina haki kutoiamini Washington.
-
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki: Makelele ya kisiasa dhidi ya Iran hayaathiri chochote
Jun 16, 2022 23:14Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran AEOI amesema: makelele ya kisiasa na mashinikizo dhidi ya Iran hayakuwa na matokeo yoyote huko nyuma na hivi sasa pia hayatakuwa na athari yoyote.
-
Uchunguzi wa maoni: Wamarekani wengi wanahisi maadili nchini mwao yamezidi kuporomoka
Jun 16, 2022 23:14Uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi mashuhuri ya Gallup unaonyesha kuwa asilimia 50 ya Wamarekani wa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa wanaitakidi kuwa thamani za maadili katika nchi hiyo zimedhoofika.
-
Kamati ya Bunge: Tuna ushahidi wa kumtia hatiani Trump
Jun 13, 2022 06:48Wanachama wa Kamati ya Bunge la Marekani inayochunguza shambulio dhidi ya jengo la Kongresi tarehe 6 Januari mwaka jana, wamesema wana ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
-
Maandamano makubwa kila pembe ya Marekani na mwito wa kuchukuliwa hatua kali zaidi za kudhibiti silaha moto
Jun 13, 2022 02:32Ongezeko kubwa la matukio ya ufyatuaji risasi dhidi ya halaiki nchini Marekani na kuongezeka pia idadi ya watu wanaouawa kwa mashambulio ya utumiaji wa silaha hizo kunakotokana na upuuzaji wa viongozi wa White House na mashinikizo ya lobi za watengezaji silaha, vimeibua wimbi kubwa la maandamano ya malalamiko ya raia wa nchi hiyo.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu kuwa mapambano ndio njia pekee ya kufikia ushindi dhidi ya Marekani
Jun 12, 2022 04:33Akizungumza jana Jumamosi alasiri katika kikao na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na ujumbe alioandamana nao, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya kusimama imara Iran na Venezuela mbele ya mashinikizo makali na vita vya pande kadhaa vya Marekani na kusisitiza: Uzoefu wa mafanikio wa nchi mbili unaonyesha kwamba njia pekee ya kukabiliana na mashinikizo hayo ni mapambano na kusimamam imara.
-
Abdollahian: Azimio la IAEA dhidi ya Iran lilichochewa kisiasa
Jun 12, 2022 03:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezikosoa vikali Marekani na nchi tatu za Ulaya za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, kwa kuwasilisha azimio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu mbele ya Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA.
-
Wamarekani waandamana kutaka kubadilishwa sheria ya kumiliki bunduki nchini humo
Jun 12, 2022 03:25Makumi ya maelfu ya watu wamefanya maandamano katika majimbo na miji mbalimbali ya Marekani ukiwemo mji mkuu Washington, kushinikiza kuangaliwa upya sheria inayoruhusu kuuzwa na kumiliki silaha za moto kiholela nchini humo; siku chache baada ya kujiri mauaji ya kutisha huko Texas, ambapo watoto 19 wa shule na walimu wawili waliuawa kwa kufyatuliwa risasi.
-
Israel yamshinikiza Biden aondea Pegasus kwenye orodha nyeusi ya US
Jun 10, 2022 22:05Maafisa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanamshinikiza Rais Joe Biden wa Marekani afute jina la kampuni ya Israel ya NSO ambayo imekuwa ikiuza programu ya kijasusi ya Pegasus kwenye orodha nyeusi ya Washington.
-
Russia yaonya kuhusu uwezekano wa makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi na kambi ya Magharibi
Jun 10, 2022 21:53Russia imezionya nchi za Magharibi kuwa hujuma ya kiintaneti dhidi ya miundomsingi yake ni jambo ambalo litaibua hatari ya kutokea makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi. Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa na kusema kuwa, miundomsingi ya kijeshi na ya baadhi ya taasisi za kiserikali nchini humo imekumbwa na hujuma ya kiintaneti ambayo imetekelezwa na makundi ya wadukuzi wa Marekani na Ukraine.