-
Waislamu Marekani waendesha mchango wa kuwasaidia Mayahudi waliouliwa kigaidi na Mkristo Robert Bowers
Oct 29, 2018 10:57Jumuiya ya Waislamu wa Marekani imefanikiwa kukusanya mchango wa makumi ya maelfu ya dola katika juhudi zao za kuwasaidia wahanga wa shambulizi la kigaidi lililotokea katika hekalu la Kiyahudi la mjini Pittsburgh na kuua watu 11 na kujeruhi wengine sita.
-
Answarullah: Marekani ndio yenye maamuzi ya kuendelea au kukomeshwa vita Yemen
Oct 29, 2018 10:24Mjumbe wa Kisiasa wa Harakati ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa, Saudi Arabia na nchi nyingine zilizoivamia nchi hiyo, zinafuata maamuzi ya Marekani katika kuendeleza au kukomeshwa vita vyao vya kichokozi nchini Yemen.
-
Trump atetea tena sheria ya kumiliki bunduki US licha ya Mayahudi 11 kuuawa Pittsburgh
Oct 28, 2018 04:36Kwa mara nyingine tena, Rais wa Marekani, Donald Trump ameunga mkono sheria inayoruhusu kuuzwa na kumiliki silaha za moto kiholela nchini humo, licha ya kuweko upinzani mkali dhidi ya sheria hiyo ya kubeba bunduki hasa baada ya mashambulizi ya silaha hizo kushadidi nchini humo.
-
Aghalabu ya Wamarekani wanataka mfumo wa vyama vingi
Oct 28, 2018 04:35Akthari ya wananchi wa Marekani wanaona kuwa mfumo wa vyama viwili vya kisiasa una mapungufu na kuna haja ya kuwa na chama au mrengo wa tatu wa kisiasa nchini humo.
-
Rais Rouhani: Iran itaipigisha magoti Marekani
Oct 27, 2018 12:12Rais Hassan Rouhani amesema kuhusu njama zinazofanywa na Marekani dhidi ya Iran, kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua makini ambazo zitaipigisha magoti Marekani.
-
Iran yaitaka dunia iheshimu uamuzi wa ICJ dhidi ya Marekani
Oct 26, 2018 10:31Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amezitaka nchi zote huru duniani kufungamana na uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ), kwa kutouinga mkono Marekani kuiwekea vikwazo Tehran.
-
Marekani, adui wa amani na usalama wa dunia
Oct 25, 2018 23:04Uamuzi uliochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani wa kujiondoa katika mkataba wa silaha za nyuklia za masafa ya kati (INF) ambao umechukuliwa katika fremu ya sera za Trump za kujiondoa katika mikataba ya kimataifa, umekabiliwa na upinzani mkubwa wa viongozi wa nchi na jumuiya mbalimbali za kimataifa.
-
Ulaya na Umoja wa Mataifa zasisitiza azma yao ya kuyalinda makubaliano ya JCPOA
Oct 25, 2018 08:28Licha ya Marekani kuyapinga makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, lakini nchi za Ulaya zinasisitiza kulindwa makubaliano hayo muhimu ya kimataifa. Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akichukua misimamo iliyo dhidi ya makubaliano hayo ambayo yalifikiwa mwezi Julai mwaka 2015 kati ya Iran na kundi la 5+1 ikiwemo marekani yenyewe na anayataja kuwa ni makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa!
-
Marekani yashindwa kuiwekea vikwazo kamili vya kibenki Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Oct 25, 2018 04:35Viongozi wa Marekani wamesema kuwa, serikali ya Rais Donald Trump hatimaye itairuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuweza kuendeleza mawasiliano yake ya kibenki kupitia mfumo wa SWIFT na kustafidi na huduma za utumaji fedha kimataifa.
-
Malengo halisi ya Marekani ya kujiondoa kwenye mkataba wa silaha za nyuklia za masafa ya kati
Oct 23, 2018 09:46Tangazo la Marekani la kujiondoa kwenye mkataba wa silaha za nyuklia za masafa ya kati lililotolewa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo limekabiliwa na radiamali nyingi hasi katika uga wa kimataifa.