Rais Rouhani: Iran itaipigisha magoti Marekani
Rais Hassan Rouhani amesema kuhusu njama zinazofanywa na Marekani dhidi ya Iran, kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua makini ambazo zitaipigisha magoti Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo bungeni katika kikao cha kujadiliwa mawaziri wanne aliowapendekeza kuongoza wizara za Barabara na Ujenzi Miji, Viwanda, Madini na Biashara, Ushirika, Kazi na Ustawi wa Jamii na Masuala ya Uchumi na Fedha.
Rais Rouhani ameashiria jinsi Marekani ilivyoshindwa na Iran katika miezi ya karibuni katika duru za kisiasa na kisheria na kueleza kwamba: Haijawahi kutokea Marekani kuchukua uamuzi muhimu katika upeo wa kimataifa dhidi ya nchi yoyote kubwa kisha ikaachwa mkono na waitifaki wake wa jadi.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa ushindi wa taifa la Iran dhidi ya Marekani ni nadra kushuhudiwa katika historia; na akaongeza kuwa: Leo dunia inalitambua taifa la Iran kuwa ni mtekelezaji wa ahadi ilizojikubalisha kuzitekeleza na inaitazama Marekani kama mkhalifu wa ahadi na pia mvunjaji sheria za kimataifa.
Rais Rouhani aidha amesema, kutokana na kuweka vikwazo katika uga mpana ambavyo vinadhuru maisha ya watu, hakuna shaka yoyote kuwa Marekani ndiye adui mkubwa zaidi wa taifa la Iran na akabainisha kwamba: Kwa hatua yake ya kutekeleza vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Iran, Marekani imeonyesha kuwa ni adui wa wananchi wa Iran.../