-
"Daesh na makundi mengine ya kitakfiri yameanzishwa na Marekani na Israel"
Jun 11, 2017 09:44Naibu Kamanda wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kundi la kigaidi la Daesh na makundi mengine ya kitakfiri yameanzishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na yamekuwa yakitumiwa na tawala hizo kwa ajili ya kufikia malengo yao.
-
Marekani yakiri askari wake watatu wameangamizwa Afghanistan
Jun 11, 2017 03:32Viongozi wa Marekani wametangaza kuwa askari watatu wa nchi hiyo wameuliwa na mwengine mmoja amejeruhiwa baada ya askari mmoja wa Afghanistan kuwafyatulia risasi wanajeshi wa Marekani huko mashariki mwa Afghanistan.
-
Marekani yaunga mkono waziwazi ISIS; Mbunge wa Congress asema: Mashambulizi ya kigaidi ya Tehran ni kwa manufaa ya Marekani
Jun 10, 2017 11:28Mbunge wa jimbo la California katika Baraza la Congress la Marekani ametoa matamshi ya kijuba na kuunga mkono waziwazi mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na genge la wakufurishaji la Daesh mjini Tehran, Iran, Jumatano asubuhi.
-
Alaeddin Boroujerdi: Marekani ni mpangaji mkuu wa njama dhidi ya Iran
Jun 09, 2017 23:27Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mashambulio ya kigaidi ya siku ya Jumatano hapa mjini Tehran na kusema kuwa, hapana shaka kuwa, mpangaji mkuu wa njama hiyo ni Marekani mtenda jinai.
-
Mbunge Marekani: Hujuma za kigaidi Tehran ni stratejia ya Trump
Jun 09, 2017 23:05Mbunge katika chama tawala cha Republican nchini Marekani amesema hujuma za hivi karibuni za kundi la kigaidi la ISIS mjini Tehran inaweza kuwa stratijia ya Rais Donald Trump.
-
Wasaudi walimuhonga Trump makumi ya maelfu ya dola ili abadili sheria ya Jasta
Jun 08, 2017 10:32Magazeti ya nchini Marekani yameandika ripoti inayofichua kwamba watawala wa Saudi Arabia, walitoa hongo ya makumi ya maelfu ya dola kwa Rais Donald Trump wa Marekani ili kumshinikiza ababadilishe sheria ya kukabiliana na waungaji mkono wa ugaidi kwa kifupi JASTA ya nchini Marekani.
-
Trump awalaumu na kuwakejeli mashahidi wa mashambulio ya Tehran
Jun 08, 2017 02:16Katika hali ambayo dunia nzima inaendelea kutoa mkono wa pole na kutuma salamu za rambirambi kufuatia mashambulio pacha ya kigaidi yaliyotokea jana hapa mjini Tehran, Rais Donald Trump wa Marekani ametoa ujumbe unaoonekana kuwalaumu na kuwakejeli mashahidi waliouawa katika hujuma hizo.
-
Putin: Hakuna atakayepona katika vita vya nyuklia vya Marekani na Russia
Jun 07, 2017 02:46Rais Vladimir Putin wa Russia ametahadharisha kuwa, iwapo Marekani itaamua kuingia katika vita vya nyuklia na nchi yake, hakuna upande utakaopona 'kusherehekea' ushindi.
-
Kerry: Makubaliano ya JCPOA hayahitaji baraka za Marekani
Jun 06, 2017 23:18Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yanaweza kuendelea kusimama imara na kutekelezwa pasina na ushiriki wa Washington.
-
Mashtaka ya Syria kwa Umoja wa Mataifa kuhusu jinai za Marekani na Daesh
Jun 06, 2017 09:44Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imetuma barua kwa nyakati tofauti kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo na kutangaza kwamba, hasara za kifedha na kiroho zilizosababishwa na mashambulio ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani dhidi ya wananchi wa nchi hiyo hazina tofauti na jinai za magaidi wa Daesh.