Jun 10, 2017 03:57 UTC
  • Alaeddin Boroujerdi: Marekani ni mpangaji mkuu wa njama dhidi ya Iran

Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mashambulio ya kigaidi ya siku ya Jumatano hapa mjini Tehran na kusema kuwa, hapana shaka kuwa, mpangaji mkuu wa njama hiyo ni Marekani mtenda jinai.

Alaeddin Boroujerdi alisema hayo jana katika hotuba yake kabla ya hotuba za Sala ya Ijumaa mjini Tehran na kubainisha kwamba, Marekani imechukia sana kutokana na kushindwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kadhia ya nyuklia  ambapo hii leo taifa hili la Kiislamu linamiliki kikamilifu teknolojia hii muhimu ulimwenguni kwa ajili ya matumizi ya amani.

Alaeddin Boroujerdi amesisitiza kuwa, serikali na wananchi wa Iran kutokana na itikadi waliyonayo na kwa mujibu wa fatuwa ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mpinduzi ya Kiislamu wameahidi kutotumia teklonojia hii kwa malengo ya kijeshi.

Shambulio la kigaidi katika jengo la Bunge

Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) ameeleza kuwa, misaada ya Iran kwa ajili ya kuhitimishwa migogoro ya Syria na Iraq ni miongoni mwa sababu kuu za njama za Marekani za kutaka kutoa pigo dhidi ya Iran.

Alaeddin Boroujerdi amesema kuwa, mashambulio ya kigaidi kama ya siku ya Jumatano mjini Tehran katu hayawezi kutia dosari yoyote irada ya taifa kubwa la Iran na mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu katika kuendelea na njia yake.

 

Tags