-
Iran yalaani maamuzi ya Rais wa Marekani
Jan 29, 2017 00:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa na kulaani vikali uamuzi wa serikali ya Marekani wa kuzuia Waislamu kuingia nchini humo ikisema kuwa, huko ni kuuvunjia heshima waziwazi ulimwengu wa Kiislamu na taifa la Iran.
-
Mfuasi wa Trump amshambulia mwanamke Mwislamu New York
Jan 27, 2017 23:18Katika tukio jingine linalothibitisha kuwa uhalifu unaotokana na chuki dhidi ya Waislamu umeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini Marekani, mfuasi wa Rais mpya wa nchi hiyo Donald Trump kutoka Massachusetts amemshambulia na kumjeruhi mwanamke Mwislamu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa John F. Kennedy mjini New York.
-
Maafisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wajiuzulu, hawataki kufanya kazi na Trump
Jan 27, 2017 00:03Maafisa wote wa ngazi za juu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani waliofanya kazi katika kipindi cha uongozi wa rais mstaafu wa nchi hiyo, Barack Obama wamejiuzulu kwa pamoja.
-
Wamarekani waandamana kupinga dikrii iliyozusha makelele ya ujenzi wa mabomba ya mafuta
Jan 25, 2017 11:49Wananchi wa Marekani wameandama kupinga agizo la Rais Donald Trump wa nchi hiyo la kutaka kuendelezwa ujenzi wa mabomba ya mafuta uliozusha upinzani na mvutano.
-
Glenn: Huenda Israel itafanya njama za kuuawa Trump wa US
Jan 24, 2017 04:45Mark Glenn, mchambuzi mashuhuri wa kisiasa nchini Marekani amesema yumkini serikali ya Washington ikapanga njama za kuuawa Rais mpya wa Marekani Donald Trump, iwapo hatasimamia maslahi ya Wazayuni.
-
Wanaoandamana kumpinga Trump sasa kutupwa jela miaka 10 au kutozwa faini nzito
Jan 23, 2017 23:26Viongozi wa Marekani wamesema kuwa, mamia ya wapinzani wanaoandamana dhidi ya Donald Trump, rais mpya wa nchi hiyo watafungwa miaka 10 jela kwa madai ya kufanya machafuko na uasi nchini humo au kulipa faini nzito.
-
Steinmeier: Kuingia Trump White House ni sawa na kufikia tamati 'Nidhamu ya Dunia'
Jan 23, 2017 05:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema, kwa kuingia Donald Trump katika Ikulu ya Marekani, White House nidhamu ya dunia ya karne ya 20 "imemalizika moja kwa moja" na hali ya mchafukoge ndiyo inayofuatia.
-
Trump awatimua mabolozi wote wa Marekani duniani
Jan 22, 2017 12:29Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa. Katika siku ya kwanza kazini, Trump ambaye aliapishwa Ijumaa kuwa rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtanguzlizi wake, Barack Obama, kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muhula wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo desturi.
-
Drone za Marekani zaua watu wanne Yemen
Jan 22, 2017 12:18Watu wanne wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma ya drone au ndege zisizo na rubani za Marekani katika mkoa wa Bayda. Duru za habari nchini Yemen zinadokeza kuwa, katika hujuma ya kwanza, kombora la drone lililenga gari lililokuwa limedaiwa kubeba watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa al-Qaeda katika wilaya ya Sawma'ah mkoani humo Jumamosi.
-
Pakistan yapinga kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Quds
Jan 19, 2017 10:55Mwakilishi wa Kudumu wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amepinga hatua yoyote ya uhamishaji wa ubalozi wa Marekani kutoka Tel-Aviv, Israel kwenda Baytul-Muqaddas na kwamba, kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.