Trump awatimua mabolozi wote wa Marekani duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24070-trump_awatimua_mabolozi_wote_wa_marekani_duniani
Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa. Katika siku ya kwanza kazini, Trump ambaye aliapishwa Ijumaa kuwa rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtanguzlizi wake, Barack Obama, kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muhula wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo desturi.
(last modified 2026-08-19T09:43:12+00:00 )
Jan 22, 2017 12:29 UTC
  • Trump awatimua mabolozi wote wa Marekani duniani

Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa. Katika siku ya kwanza kazini, Trump ambaye aliapishwa Ijumaa kuwa rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtanguzlizi wake, Barack Obama, kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muhula wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo desturi.

Zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbali mbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana punde baada ya Trump kuapishwa.

Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na waitifaki muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza, Canada. Inatabiriwa kuwa nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Kongresi kabla ya kuanza kazi zao.

Maandamano ya kumpinga Trump

Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani. Hayo yanajiri huku maandamano yakiripotiwa kote duniani dhidi ya kiongozi huyo. Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu. Aidha kumefanyika maandamano 637 katika maeneo mbali mbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais mpya wa Marekani.