Drone za Marekani zaua watu wanne Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24064-drone_za_marekani_zaua_watu_wanne_yemen
Watu wanne wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma ya drone au ndege zisizo na rubani za Marekani katika mkoa wa Bayda. Duru za habari nchini Yemen zinadokeza kuwa, katika hujuma ya kwanza, kombora la drone lililenga gari lililokuwa limedaiwa kubeba watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa al-Qaeda katika wilaya ya Sawma'ah mkoani humo Jumamosi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 22, 2017 12:18 UTC
  • Drone za Marekani zaua watu wanne Yemen

Watu wanne wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma ya drone au ndege zisizo na rubani za Marekani katika mkoa wa Bayda. Duru za habari nchini Yemen zinadokeza kuwa, katika hujuma ya kwanza, kombora la drone lililenga gari lililokuwa limedaiwa kubeba watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa al-Qaeda katika wilaya ya Sawma'ah mkoani humo Jumamosi.

Siku moja kabla, drone nyingine ya Marekani inadaiwa kulenga mtaalamu wa kijeshi wa kundi hilo la kigaidi katika mkoa huo huo. Kati ya wanaoripotiwa kuuawa ni Abu Anis al-Abi ambaye anadaiwa kuwa ni mmoja kati ya makamanda wa al Qaeda nchini Yemen.

Mashambulio ya droni mara nyingi huua raia wa kawaida

Ndege zisizo na rubani za Marekani zimekuwa zikitumiwa kushambulia maeneo mbalimbali nchini Somalia na pia katika nchi zingine za Kiislamu kama vile Afghanistan, Yemen, Libya na Pakistan. Umoja wa Mataifa unailaumu Marekani kwa mauaji yanayofanywa na ndege zisizo na rubani za nchi hiyo katika nchi mbalimbali ukisema kuwa yanakiuka sheria za kimataifa. Marekani inadai kuwa inawalenga magaidi katika oparesheni zake lakini aghalabu ya watu wanaouawa katika hujuma hizo za ndege za kivita za Marekani ni raia wa kawaida.