-
Wamarekani waanza kuisakama Saudia juu ya shambulio la Septemba 11
Oct 01, 2016 04:23Mjane wa Kimarekani ambaye mumewe aliuawa katika shambulizi la Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani ameipeleka mahakamani serikali ya Saudi Arabia kwa kuhusika na hujuma hiyo, sambamba na kutaka kulipwa fidia kutokana na mauaji ya mumewe.
-
Russia: Kauli ya Marekani ni dhihirisho kuwa inaunga mkono ugaidi
Sep 29, 2016 10:50Serikali ya Moscow imesema matamshi ya hivi karibuni ya Marekani kuwa magaidi wa Daesh wanaofanya mashambulizi dhidi ya Syria yumkini wakaanza kuishambulia miji ya Russia ni ithibati tosha kuwa Washington inaunga mkono ugaidi.
-
Mgombea urais wa chama cha Kijani US: Trump na Clinton ni hatari sana kwa dunia
Sep 27, 2016 11:31Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha kijani katika uchaguzi wa rais nchini Marekani, amewakosoa vikali wagombea wa vyama vya Republican na Democrat katika siasa za kigeni za nchi hiyo akisema kuwa ni watu hatari sana.
-
Russia yakosoa vikali matamshi ya Marekani na Magharibi katika Umoja wa Mataifa
Sep 26, 2016 11:02Russia imekosoa matamshi yaliyotolewa na Mabalozi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa katika Umoja wa Mataifa kwa mashambulizi ya jeshi la Russia katika ngome za makundi ya kigaidi huko Syria.
-
Zarif: Kubaki tawala za baadhi ya nchi kumefungamana na utegemezi wao kwa Marekani
Sep 25, 2016 12:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema tawala za baadhi ya nchi za eneo zinahisi uhalali wao na kuendelea kubaki kwao kunategemea bawa la hifadhi na uungaji mkono wa Marekani.
-
Ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi katika historia ya Marekani
Sep 25, 2016 08:22Huku mjadala wa ubaguzi wa rangi dhidi ya jamii ya watu weusi nchini Marekani hususan kufuatia mashambulizi ya polisi dhidi yao ukiendelea kugonga vichwa vya habari, rais wa nchi hiyo ameibuka na kusema kuwa, historia ya Wamarekani imejaa vipindi vya giza na mwanga.
-
Sudan Kusini yailaumu Marekani kwa kuendelea kuiwekea vikwazo
Sep 24, 2016 01:19Serikali ya Sudan Kusini imeilaumu Marekani kwa siasa zake zisizo sahihi kuhusiana na nchi hiyo na kusema, Juba inahitajia misaada mbalimbali ikiwemo ya silaha na si vikwazo.
-
Iran yaionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani
Sep 24, 2016 01:10Kamanda wa ngazi za juu nchini Iran amesema vikosi vya ulinzi wa angani nchini vimeionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya U2 ambayo ilikuwa inajaribu kuruka katika mipaka ya Iran.
-
Rais Rouhani: Utendaji wa Marekani ni kinyume cha mapatano ya nyuklia
Sep 23, 2016 10:26Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, tume ya pamoja ya kuratibu mapatano ya nyuklia, maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), imesema utendaji wa Marekani ni kinyume cha mapatano hayo.
-
Marekani imepoteza maelfu ya mabilioni ya dola kwa kisingizio cha mashambulizi ya Septemba 11
Sep 19, 2016 22:14Matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu kimoja nchini Marekani yanaonyesha kuwa Washington imepoteza dola bilioni elfu tano kwa kile ilichokiita mapambano dhidi ya ugaidi, tangu kutokea mashambulizi ya Septemba 11 nchini humo.