Iran yaionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i15937-iran_yaionya_na_kuitimua_ndege_ya_kijasusi_ya_marekani
Kamanda wa ngazi za juu nchini Iran amesema vikosi vya ulinzi wa angani nchini vimeionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya U2 ambayo ilikuwa inajaribu kuruka katika mipaka ya Iran.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Sep 24, 2016 01:10 UTC
  • Iran yaionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani

Kamanda wa ngazi za juu nchini Iran amesema vikosi vya ulinzi wa angani nchini vimeionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya U2 ambayo ilikuwa inajaribu kuruka katika mipaka ya Iran.

Brigedia Jenerali Farzad Ismaili, kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Ambiya SAW amesea hivi, karibuni walinzi wa anga nchini waliitambua ndege ya kijasusi ya Marekani iliyokuwa inajaribu kujipenyeza nchini Iran na kuilazimisha kurejea ilikotoka.

Kamanda huyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu ni wapi ndege hiyo ilikuwa ikijaribu kuingia anga ya Iran.

Ndege ya Lockheed U2 yenye lakabi ya 'Dragon Lady'  ni dege ya Marekani yenye injini moja na yenye uwezo wa kuruka masafaa ya juu sana kwa malengo ya kijasusi na inatumiwa na Jeshi la Angani la Marekani. Ndege hiyo ina uwezo wa kukusanya habari za kijasusi usiku na mchana na katika hali zote za hewa huki ikiwa na kamera za hali ya juu sana.

Ndege ya Kijasusi ya Marekani aina ya RQ-170 Sentinel iliyolazimishwa kuteremka chini na vikosi vya Iran mnamo Desemba 2011

Mwezi Agosti pia Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Ambiya SAW kiliionya na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani ambayo ilijaribui kuingia katika anga ya Iran. Rada za Iran ziliweza kuitambua ndege hiyo pamoja na kuwa Wamarekani wanadai kuwa haiwezi kuonekana kwenye rada.

Iran kwa mara kadhaa sasa imefanikiwa kuziangusha ndege za kijasusi za Marekani zilizokuwa zimekiuka anga ya nchi hii huku ikizionya na kuzitimua zile zilizokuwa zimekaribia mipaka ya nchi hii.