-
Jenerali Ashtiani: US itakabiliwa na pigo zito iwapo vita vya Gaza havitamalizika
Nov 05, 2023 23:29Waziri wa Ulinzi wa Iran ameonya kuwa, Marekani itakabiliwa na pigo kubwa na zito iwapo itashindwa kusimamisha mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Mbunge wa Marekani asema: Biden anasaidia mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina
Nov 04, 2023 23:00Mbunge mmoja wa Baraza la Congress ya Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic amesema kuwa, rais wa nchi hiyo, Joe Biden anasaidia moja kwa moja mauaji ya umati na maangamizi ya kizazi dhidi ya Wapalestina na kwamba Wamarekani hawatolisahau hilo katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2024.
-
Hitilafu kati ya Warepublican and White House kuhusu msaada kwa Israel na Ukraine
Nov 04, 2023 22:55Katika hali ambayo serikali ya Biden imetangaza kuunga mkono kikamilifu jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Ghaza na hata kupinga usitishaji vita, lakini suala la msaada wa kifedha kwa Israel ambalo linatiliwa maanani na Warepublican sambamba na mtazamo wa White ambayo inataka kutolewa kwa wakati mmoja misaada ya fedha na silaha kwa Ukraine limezusha hitilafu kubwa kati ya Kongresi na White House.
-
Kambi za kijeshi za Marekani zashambuliwa kwa droni Iraq, Syria
Nov 03, 2023 23:33Vituo viwili vya kijeshi vya Marekani vimeshambuliwa katika hujuma za ndege zisizo na rubani (droni) katika eneo la Kurdistan la kaskazini mwa Iraq na katika mkoa wa Hasaka, mashariki mwa Syria.
-
Hamas yasema Marekani inawasaidia Wazayuni katika vita vya Ghaza
Nov 02, 2023 02:49Mmoja wa viongozi wa kundi la Wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina Hamas amesema Marekani inaunga mkono na kuusaidia kwa hali na mali Utawala wa Kizayuni katika mapigano ya Ghaza.
-
"Okoa watoto wa Gaza", Wamarekani wakatiza kikao cha Kongresi cha kumsaili Blinken na Austin
Nov 01, 2023 04:45Waandamanaji jana Jumanne walikatiza kikao cha kuwahoji mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Marekani katika Bunge la Kongresi kilichoitishwa kwa ajiili ya kijadili suala la kuongeza uungaji mkono na misaada kwa Israel na Ukraine. Waandamanaji hao walioingia ndani ya Kongresi walitoa nara wakitaka "kuokolewa watoto wa Gaza" na "kusitishwa mapigano mara moja" katika eneo hilo la Palestina.
-
Hatua mpya za Marekani katika fremu ya kuuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel
Oct 30, 2023 08:05Tangu kuanza duru mpya ya vita kati ya utawala wa Kizayuni na makundi ya muqawama ya Palestina na operesheni ya Kimbunga ya Al-Aqsa na radiamali kali ya Wazayuni dhidi ya hatua hiyo, Marekani ikiwa mshirika wa kistratijia wa Israel imetoa himaya kubwa ya kisiasa, kidiplomasia na kijeshi kwa utawala huo ghasibu. Filihali Washington imechukua hatua mpya katika mwelekeo huu.
-
Vita vya Ukraine na Ghaza vinavyozidi kuyanufaisha makampuni ya silaha ya Marekani
Oct 30, 2023 04:13Vita nchini Ukraine vinaendelea sambamba na kuongezeka mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza huko Palestina huku ripoti zikisema kuwa, viwanda vya kuzalisha silaha vya nchini Marekani vinafaidika mno na vita hivyo.
-
Jarida lathibitisha: Vikosi maalumu vya Marekani vinapigana bega kwa bega na Wazayuni katika vita vya Gaza
Oct 28, 2023 23:30Jarida la Marekani linalohusika na masuala ya kijeshi limefichua kuwa vikosi maalumu vya nchi hiyo vinapigana bega kwa bega na Wazayuni katika vita vya Gaza.
-
Kupigiwa kura ya veto maazimio yanayohusu vita vya Ghaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Oct 27, 2023 03:57Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limeshindwa kupasisha azimio Katika hali ambayo wananchi wa Ukanda wa Ghaza bado wanakabiliwa na mashambulizi ya kinyama na ya kutisha ya utawala wa Kizayuni ambapo utawala huo unazuia kufikishwa misaada ya dharura katika eneo hilo.