-
Vyama vya siasa Misri vyalaani shambulizi la kigaidi dhidi ya Msikiti wa al Rawdhah
Nov 26, 2017 04:51Vyama mbalimbali vya kisiasa nchini Misri vimelaani shambulizi la kigaidi dhidi ya Msikiti wa al Rawdhah katika mji wa al Arish makao makuu ya mkoa wa Sinai Kaskazini na kutangaza kuwa kuna njama zinatekelezwa kutoka nje ili kuzusha hali ya mchafukoge nchini humo.
-
Serikali ya Ufaransa yawawekea Waislamu vizuizi vipya wasiweze kusali Sala ya Ijumaa katika mji wa Paris
Nov 20, 2017 04:15Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerard Collomb amesema ni marufuku kusali Sala la Ijumaa katika eneo la Clichy kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.
-
Imarati yazitaka nchi za Ulaya zidhibiti misikiti kwa kuweka CCTV
Nov 15, 2017 04:15Waziri mmoja wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ameitaka Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya kudhibiti misikiti na makhatibu wa misikiti katika nchi zao kwa shabaha ya kuzuia uenezwaji wa misimamo mikali ya kufurutu ada.
-
Binti wa miaka 13 aua watu 5 katika shambulio dhidi ya msikiti Cameroon
Sep 14, 2017 10:09Mshambuliaji aliyekuwa amejifunga bomu amejiripua na kuua watu wasiopungua watano katika msikiti mmoja ulioko kaskazini mwa Cameroon karibu na mpaka wa nchi hiyo na Nigeria.
-
Vituo viwili vya Kiislamu vyashambuliwa na kundi lenye chuki za kidini Uhispania
Aug 21, 2017 03:46Vituo viwili vya Kiislamu vimeshambuliwa na kundi la watu wenye chuki dhidi ya dini ya Kiislamu nchini Uhispania.
-
Jenerali Qassem Soleimani: Iran ni chemchemu ya uthabiti katika eneo
Aug 20, 2017 22:01Kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Iran haijawahi katu kuzusha mgogoro na kulea utakfiri; na leo hii imekuwa chemchemu ya uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Watu 8 wajeruhiwa katika hujuma msikitini Ufaransa
Jul 03, 2017 03:30Watu 8 wamejeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi mbele ya mlango ya msikiti kusini mwa Ufaransa.
-
Azerbaijan yazidi kuwakandamiza Waislamu, yabomoa msikiti mwingine wa kihistoria Baku
Jul 02, 2017 23:14Serikali ya Azerbaijan imeendeleza ukandamizaji wake dhidi ya Waislamu ambapo katika tukio la karibuni kabisa imebomoa msikiti mwingine wa kihistoria wa Baku, mji mkuu wa nchi hiyo kwa kisingizio cha kuwalinda waumini wanaoswali ndani yake.
-
Ukarabati wa msikiti mkubwa zaidi wa udongo wakamilika nchini Mali
May 12, 2017 22:04Mamia ya wananchi Waislamu wa Mali wamekamilisha kazi ya matengenezo ya msikiti mkubwa zaidi wa matofali ya udongo duniani ulioko mjini Djenné kusini mwa nchi hiyo.
-
Marekani yakiri kuhusika na shambulizi dhidi ya msikiti nchini Syria
May 05, 2017 09:07Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) hatimaye imekiri kuwa ndege za kijeshi za US zilitekeleza shambulizi a anga dhidi ya msikiti mmoja nchini Syria ambapo makumi ya watu waliuawa.