Jul 03, 2017 03:44 UTC
  • Azerbaijan yazidi kuwakandamiza Waislamu, yabomoa msikiti mwingine wa kihistoria Baku

Serikali ya Azerbaijan imeendeleza ukandamizaji wake dhidi ya Waislamu ambapo katika tukio la karibuni kabisa imebomoa msikiti mwingine wa kihistoria wa Baku, mji mkuu wa nchi hiyo kwa kisingizio cha kuwalinda waumini wanaoswali ndani yake.

Maafisa wa usalama wa nchi hiyo waliubomoa msikiti huo wa kihistoria unaojulikana kwa jina la Hajj Jawad, jioni ya Jumamosi kwa madai kuwa msikiti huo ungeweza kuhatarisha maisha ya waumini wanaoutumia kuswali, madai ambayo yamepingwa vikali na raia wa nchi hiyo.

Misikiti mikongwe inayokabiliwa na bomoabomoa ya serikali ya  Azerbaijan

Mwezi Aprili mwaka huu, meya wa mji wa Baku alitangaza azma ya kubomoa msikiti huo wa kihistoria, hata hivyo kutokana na malalamiko makali ya Waislamu, akalazimika kusitisha lengo lake hilo. Huo ni msikiti wa pili wa kihistoria kubomolewa nchini Azerbaijan ndani ya kipindi kisichofika miezi mitatu. Tarehe 11 Aprili mwaka huu serikali ya nchi hiyo ilibomoa msikiti mwingine wa kihistoria wa 'Hajj Abd al-Rahim Bike' mjini Baku kwa madai kwamba msikiti huo ulikuwa katika eneo la ramani mpya ya maendeleo ya manispaa ya jiji hilo. Hii ni katika hali ambayo misikiti hiyo iko katika orodha ya athari za kihistoria za Wizara ya Utamaduni ya Azerbaijan.

Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan, mshirika wa Marekani na Israel

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali kwa kushirikiana na bunge la nchi hiyo imeshadidisha hatua za ukandamizaji dhidi ya Waislamu hususan Waislamu wa Kishia ambao wanaunda asilimia kubwa ya wakazi wa taifa hilo la Asia Magharibi. Kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na serikali ya mji mkuu wa nchi hiyo Baku, ni makosa wasomi waliosomea katika baadhi ya nchi za Kiislamu kama vile Iran kusalisha swala ya jamaa mjini hapo. Ukandamizaji wa serikali ya Azerbaijan unajumuisha kuwatia jela zaidi ya viongozi wa kiroho 200 na mubalighina wa Kiislamu.

Tags