Nigeria yapinga madai ya Trump kuhusu mauaji ya Wakristo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i132828-nigeria_yapinga_madai_ya_trump_kuhusu_mauaji_ya_wakristo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar, amepinga madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mauaji ya Wakristo nchini Nigeria, akionya dhidi ya kauli zinazoweza kuchochea mgawanyiko wa kidini au kikabila nchini humo.
(last modified 2025-11-05T12:37:04+00:00 )
Nov 05, 2025 12:37 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar,
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar,

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Tuggar, amepinga madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mauaji ya Wakristo nchini Nigeria, akionya dhidi ya kauli zinazoweza kuchochea mgawanyiko wa kidini au kikabila nchini humo.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin, Tuggar aliwaonesha waandishi hati iliyopewa jina “Ahadi ya Katiba ya Nigeria kuhusu Uhuru wa Kidini na Utawala wa Sheria”, akieleza kuwa hati hiyo inaeleza wazi msimamo wa katiba ya Nigeria kuhusu uhuru wa kuabudu.

Wakati wa mkutano wa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann Wadephul, Tuggar alisema: “Hii inaonesha kuwa haiwezekani kuwepo kwa mateso ya kidini yanayoungwa mkono kwa namna yoyote na serikali ya Nigeria katika ngazi yoyote.”

Trump alitangaza Nigeria kuwa “Nchi ya Wasiwasi Maalum” siku ya Jumamosi, akionya kuhusu uwezekano wa kuishambulia kijeshi ili “kuwalinda” Wakristo. Alidai kuwa “idadi kubwa” ya Wakristo wanauawa nchini Nigeria.

Hatua hiyo ilikuja baada ya ombi kwa utawala wa Trump kutoka kwa Mbunge wa Marekani Riley Moore, aliyedai kuwa zaidi ya Wakristo 7,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka huu pekee, huku mamia wakitekwa nyara, kuteswa au kufurushwa na makundi ya kigaidi. Seneta Ted Cruz pia aliishutumu serikali ya Nigeria kwa kuruhusu “mauaji ya halaiki” dhidi ya Wakristo na kuwasilisha mswada wa sheria unaolenga kuwawekea vikwazo maafisa wa Nigeria. Kwa mujibu wa Cruz, Wakristo 50,000 wameuawa nchini Nigeria tangu mwaka 2009, na shule 2,000 pamoja na makanisa 18,000 kuharibiwa na magaidi aliowataja kuwa Waislamu.

Maafisa wa Nigeria wamekiri kuwa nchi hiyo inakabiliwa na changamoto za kiusalama zinazohusiana na makundi ya kigaidi ya Boko Haram na ISIS Kanda ya Afrika Magharibi (ISWAP).

Siku ya Jumamosi, Rais wa Nigeria Bola Tinubu alisema kuwa serikali yake “inapinga mateso ya kidini na haiyachochei."

Hata hivyo, Nigeria imekosoa vitisho vya Marekani kuishambulia kijeshi nchi hiyo.. Daniel Bwala, mshauri maalum wa Rais Tinubu, aliambia RT katika mahojiano maalum kuwa Washington inapaswa