Jul 03, 2017 08:00 UTC
  • Watu 8 wajeruhiwa katika hujuma msikitini Ufaransa

Watu 8 wamejeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi mbele ya mlango ya msikiti kusini mwa Ufaransa.

Taarifa zinasema watu wenye silaha waliwafyatulia risasi Waislamu walipokuwa wakiondoka katika Msikiti wa  Ar Rahma eneo  la Avignon Jumapili usiku.

Taarifa zinasema, hujuma hiyo imetekelezwa na watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao ambapo waliwafyatulia risasi Waislamu katika mlango wa msikiti na kuwajeruhi wanane akiwemo binti mwenye umri wa miaka saba.

Idara ya Mwendesha Mashtaka Ufaransa imedai kuwa, tukio hilo si la kigaidi na eti kwamba msikiti huo haukulengwa na kuongeza kuwa, ulikuwa ni mzozo baina ya vijana

Polisi wanasema hawajaweza kuwatambua washambuliaji hao na kwamba uchunguzi unaendelea.

Tukio hilo limeibua wasiwasi miongoni mwa Waislamu Ufaransa ambao hivi karibuni walisuhudia pia mtu moja akijaribu kuwakanyaga Waislamu kwa gari nje ya msikiti mmoja kusini mashariki mwa Paris.

Msikiti wa Finsbury Park mjini London

Katika wiki za hivi karibuni bara Ulaya limeshuhudia vitendo kadhaa vya hujuma dhidi ya Waislamu. Katika sikukuu ya Idul Fitr mjini Newcastle, Waislamu waliokuwa wakiswali walishambuliwa huku gari likiwajeruhi Waislamu waliokuwa wakitoka msikitini mjini London huku katika msikiti wa Finsbury Park na mtu moja kupoteza maisha katika usiku wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Aidha hivi karibuni pia mashariki mwa London Waislamu wawili walimiminiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Tags