Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametoa amri ya kuongezwa idadi ya askari kwenye eneo lililo na utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta ambalo limekuwa likishuhudia machafuko kwa muda sasa.
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limepata mafanikio makubwa katika operesheni yake ya pamoja na jeshi la Cameroon dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram.
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametangaza kuwa, ataliweka katika mipango ya serikali yake suala la kukabiliana na vitisho vya waasi wa eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Nigeria amesisitiza juu ya udharura wa kutekeleza operesheni imara za kijasusi dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram.
Nchi kadhaa za magharibi mwa Afrika zilizoanzisha muungano wa kijeshi wa kupambana na Boko Haram zinakosolewa kutokana na kushindwa kulitokomeza kundi hilo la kigaidi.
Televisheni ya Ufaransa imeonesha picha za kaburi la umati la Waislamu wa madhehebu ya Shia waliouawa kinyama mwishoni mwa mwaka jana na jeshi la Nigeria.
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imeishtaki serikali na jeshi la nchi hiyo kwa kuendelea kumshikilia kinyume cha sheria kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Angola hivi sasa imekuwa nchi ya kwanza inayozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika.
Mwanaharakati mmoja maarufu wa nchini Uingereza amekosoa vikali ukimya wa jamii ya kimataifa juu ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu nchini Nigeria.
Polisi ya Nigeria imewatia mbaroni makamanda wawili wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram katika jimbo la Taraba, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.