-
WHO yatangaza mlipuko mpya wa ugonjwa wa Polio nchini Niger
Apr 29, 2020 08:12Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa Niger imekumbwa na mlipuko mpya wa ugonjwa wa kupooza viungo vya mwili wa Polio, baada ya kusimamishwa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo kufuatia mlipuko wa janga la Corona.
-
Magaidi 50 wa kundi la Boko Haram wauawa huko Niger
Mar 18, 2020 02:34Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza kuwa magaidi hamsini wanachama wa kundi la Boko Haram wameangamizwa huko kusini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Magaidi 120 wauawa kusini magharibi mwa Niger
Feb 22, 2020 03:53Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza habari ya kuuawa magaidi 120 na kutekwa magari na vifaa vyao vya kutengenezea mabomu katika operesheni maalumu iliyofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo katika eneo la kusini magharibi mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
UNICEF: Waniger milioni 3 wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu
Feb 20, 2020 03:00Ripoti iliyotolewa na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema kuwa karibu wanawake na watoto milioni tatu wa Niger wanahitajia misaada ya dharura wa kibinadamu.
-
Watu 23 wapoteza maisha wakigombania chakula Niger
Feb 18, 2020 04:27Kwa akali watu 23 wameuawa katika mkanyagano wa kugombania chakula cha msaada nchini Niger.
-
Rais wa Niger amfuta kazi Mkuu wa Majeshi baada ya kuuawa askari 174
Jan 14, 2020 08:30Rais Issoufou Mahamadou wa Niger amempiga kalamu nyekundu Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Luteni Jenerali Ahmed Mohamed kufuatia mashambulio ya magenge ya kigaidi na waasi yaliyoua askari 174 wa nchi hiyo tokea mwezi Disemba mwaka uliomalizika wa 2019 hadi sasa.
-
Mapigano mapya yaua watu 14 magharibi mwa Niger
Dec 27, 2019 21:01Watu wenye silaha wameshambulia msafara wa magari ya kijeshi katika eneo la Tillabéri la magharibi mwa Niger na kuua watu wasiopungua 14.
-
17 wauawa katika mapigano na magaidi magharibi mwa Niger
Dec 11, 2019 08:51Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza kuwa wanajeshi watatu wa nchi hiyo na magaidi 14 wameuawa katika shambulizo la kundi moja la kigaidi kwenye kambi ya jeshi magharibi mwa nchi.
-
Wanajeshi 12 wa Niger wauawa katika shambulio la Boko Haram
Oct 31, 2019 04:27Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza kuwa, wanajeshi 12 wa nchi hiyo wameuawa baada ya kambi yao kushambuliwa na kundi la kigaidi la Boko Haram kusini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Maelfu ya watu wamekuwa wakimbizi nchini Niger kutokana na mafuriko
Oct 21, 2019 23:51Mafuriko yaliyoyaathiri maeneo ya kusini mashariki mwa Niger tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba hadi sasa yamesaabisha watu elfu 23 kukosa makazi.