17 wauawa katika mapigano na magaidi magharibi mwa Niger
(last modified Wed, 11 Dec 2019 12:21:10 GMT )
Dec 11, 2019 12:21 UTC
  • 17 wauawa katika mapigano na magaidi magharibi mwa Niger

Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza kuwa wanajeshi watatu wa nchi hiyo na magaidi 14 wameuawa katika shambulizo la kundi moja la kigaidi kwenye kambi ya jeshi magharibi mwa nchi.

Shambulio hilo lilitekelezwa jana na kundi moja la kigaidi katika kambi ya jeshi huko Tahoua magharibi mwa Niger. Eneo hilo linapatikana karibu na mpaka wa Mali. Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Niger imeeleza kuwa magaidi hao walivamia kambi hiyo ya jeshi huko Tahoua huku wakiwa na magari 12 hata hivyo walalazimika kukimbilia Mali baada ya kukabiliwa na jeshi. Serikali ya Niger jana usiku ilitangaza kurefusha muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi mingine mitatu. Hali hiyo ya hatari ilitangazwa tangu mwaka juzi 2017.  

Kundi la kigaidi la Boko Haram katika miaka ya karibuni limefanya mashambulizi mengi huko Nigeria na katika nchi jirani zake ikiwemo Niger. 

Hujuma za kundi la kigaidi la Boko Haram Nigeria

Kundi hilo lilibeba silaha tangu mwaka 2009 ili kujiimarisha huko kaskazini mwa Nigeria na kisha likaeneza mashambulizi hayo huko Niger, Chad na kaskazini mwa Cameroon. 

 

Tags