UNICEF: Waniger milioni 3 wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu
(last modified Thu, 20 Feb 2020 06:30:13 GMT )
Feb 20, 2020 06:30 UTC
  • UNICEF: Waniger milioni 3 wanahitajia misaada ya dharura ya kibinadamu

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema kuwa karibu wanawake na watoto milioni tatu wa Niger wanahitajia misaada ya dharura wa kibinadamu.

Taarifa ya UNICEF imesema kuwa, raia karibu milioni tatu wa Niger ambao zaidi ya nusu yao ni watoto, wanahitajia misaada ya dharura. Shirika hilo limetoa wito wa kutiliwa maanani hali mbaya ya watoto hao na familia zao na kuongeza kuwa: Hali mbaya ya ukosefu wa usalama inayoshuhudiwa katika mpaka wa nchi hiyo na Nigeria imewalazimisha makumi ya maelfu ya wanavijiji kuwa wakimbizi.

Taarifa ya UNICEF imeongeza kuwa mashambulizi yanayofanywa dhidi ya raia katika eneo la Ziwa Chad yanazuia wakimbizi laki 2 na 63 elfu kurejea katika makazi yao katika eneo la Difa.  

UNICEF: Wakimbizi wanahitajia misaada ya dharura eneo la Ziwa Chad

Kuongezeka kwa mashambulizi ya makundi ya wanamgambo na waasi katika nchi za Niger, Mali na Cameroon kumesababisha mauaji ya makumi ya watu na kuwalazimisha maelfu ya wengine kuwa wakimbizi.

Kundi kubwa zaidi linalofanya mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo hilo la Afrika ni lile la Boko Haram. 

Tags