-
Onyo la UN kuhusu ongezeko la vyama vya mrengo wa kulia barani Ulaya
Jul 06, 2024 02:36Volker Turk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, alionya Jumatano wiki hii kuhusu kuibuka kwa vyama vya mrengo wa kulia vyenye misimamo ya kufurutu mipaka barani Ulaya na kuhatarishwa haki za wahamiaji na wakimbizi.
-
Umoja wa Mataifa watoa onyo kali kuhusu kuongezeka majanga katika Ukanda wa Gaza
Jun 21, 2024 02:14Francesca Albanese, Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, amesema katika taarifa kwamba hali ya maafa huko Ukanda wa Gaza imezidi kuwa mbaya. Kwa kauli yake, utawala haramu wa Israel unalenga misafara ya misaada ya kibinadamu inayotumwa Gaza na kuzuia ufikaji wa misaada katika ukanda huo.
-
Onyo jipya kuhusu kuingia NATO katika vita vya Ukraine
Apr 23, 2024 04:25Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Hungary amesema katika taarifa kwamba viongozi wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya Kijeshi ya Magharibi (NATO) wanauchukulia mzozo wa Moscow na Kyiv kuwa ni wao na wala hawazingatii hatari ya kujihusisha na mzozo huo. Ameonya kuwa NATO inakaribia kutuma askari wake huko Ukraine.
-
Onyo la Iran kwa Marekani na Magharibi kuhusu madhara yatakayozipata zikiiunga mkono Israel
Apr 15, 2024 12:02Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeionya na kuitahadharisha Marekani na nchi za Magharibi juu ya kuuunga mkono kijeshi utawala wa Kizayuni na kufanya chokochoko dhidi ya Iran na kutangaza kwamba, iwapo nchi hizo zitaingilia kati katika kuuunga mkono utawala wa Kizayuni, vituo vyao vyote na maeneo yote ya maslahi yao yatashambuliwa na vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Ushindi wa mtetezi wa Palestina katika uchaguzi wa Bunge la Uingereza na onyo kali la Sunak
Mar 03, 2024 02:15Licha ya kuwa Uingereza inahesabiwa kuwa ni miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini mielekeo ya kisiasa na kijamii inaashiria kwamba waungaji mkono wa Wapalestina wanazidi kupata nguvu katika nchi hiyo ya Ulaya, suala ambalo limeibua onyo la Waziri Mkuu wa kihafidhina wa Uingereza, Rishi Sunak.
-
Indhari ya Uhispania kuhusu matukio ya eneo na ya kimataifa ya vita vya Gaza
Jan 19, 2024 03:27Pedro Sánchez, Waziri Mkuu wa Uhispania ameonya kuwa, usalama na uthabiti wa eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) umekuwa hatarini na kwamba, mashambulizi haya yanahatarisha nidhamu na uratibu wa ushirikiano wa pande kadhaa.
-
Onyo la Moscow kuhusu kuendelea vita vya Ukraine mwaka 2024
Dec 01, 2023 07:59Licha ya kupita karibu miezi 22 tangu kuanza vita vya umwagaji damu nchini Ukraine, lakini hakuna matumaini yoyote yanayoashiria kumalizika mzozo huo hivi karibuni. Hii ni katika hali ambayo nchi za Magharibi kwa sasa zimeshughulishwa na vita vya Gaza na hivyo kutozingatia sana vita vya Ukraine, jambo ambalo limeipelekea serikali yenye mielekeo ya Kimagharibi ya Kyiv kukata tamaa kuhusu kupata misaada zaidi ya nchi hizo.
-
Indhari ya Borrell kuhusu uwezekano wa kusambaratika Umoja wa Ulaya
Sep 24, 2023 02:20Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametahadharisha kuwa umoja huo unakabiliwa na mgawanyiko mkubwa kuhusu sera za uhamiaji na kwamba suala hilo linaweza kuufanya Umoja wa Ulaya uvunjike.
-
Onyo la Russia kuhusu kuzuka vita vya nyuklia kufuatia ongezeko la kutumwa silaha za Magharibi nchini Ukraine
Mar 25, 2023 02:18Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Russia, ameonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vya nyuklia, akisema kuendelea kutumwa silaha nchini Ukraine kunaongeza maradufu uwezekano wa kuibuka hivi karibuni vita vya nyuklia karibu katika eneo.
-
Onyo la Putin kuhusu kukithiri kwa vitisho vya kigaidi nchini Afghanistan
Feb 12, 2023 02:34Rais wa Russia, Vladimir Putin amesema kwamba: "Tishio la ugaidi limeongezeka baada ya Marekani kuondoka Afghanistan."