-
Arab League yatahadharisha:Jamii ya kimataifa imepuuza kadhia ya Palestina
Jun 14, 2023 04:14Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ametahadharisha kuhusu hatua ya jamii ya kimataifa ya kupuuza suala la Palestina chini ya kivuli cha utawala wa Kizayuni wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia.
-
China: Tutaendelea kuunga mkono kadhia ya Palestina
Jun 12, 2023 01:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China amesema Beijing itaendelea kuunga mkono mapambano halali ya Wapalestina ya kupigania haki zao za kitaifa, na kusisitiza kwamba kadhia ya Palestina ni katika masuala muhimu ya eneo la Asia Magharibi.
-
Mpango wa mashirika 100 ya Kimarekani wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi wa utawala wa Israel
Jun 09, 2023 22:12Mashirika mia moja ya Kimarekani yameanzisha mpango uliopewa jina la "Jamii Zisizo na Ubaguzi wa Rangi" kwa lengo la kusitisha uungaji mkono wa nchi yao kwa utawala wa kibaguzi wa Israel.
-
UN 'yaguswa' na ukatili wa Israel wa kumuua mtoto wa miaka 2
Jun 06, 2023 02:09Umoja wa Mataifa umelaani mauaji ya mtoto mdogo wa Kipalestina yaliyofanywa na vyombo vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mexico yaupandishia hadhi ubalozi wa Palestina nchini humo
Jun 04, 2023 07:55Mexico imechukua hatua ya kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Palestina, na sasa ofisi ya mahusiano ya Palestina katika nchi hiyo ya Amerika ya Latini imepandishwa ngazi na kuwa ubalozi kamili.
-
Al-Qaddumi: Kadhia ya Palestina ni kipaumbele cha sera za nje za Iran
Jun 03, 2023 02:47Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nchini Iran amesema kuwa, kwa miaka mingi sasa baada ya kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kadhia ya Palestina imeendelea kuwa kipaumbele cha sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu.
-
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Palestina yaonya upanuzi wa vitongoji vya walowezi Nablos
May 31, 2023 03:17Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya mamlaka ya ndani ya Palestina imeonya kuhusiana na upanuzi wa vitongojii vya walowezi wa Kizayuni huko Nablos, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Jebeli: Kuweza Muqawama wa Palestina kuushurutisha utawala wa Kizayuni ni ushindi mkubwa
May 30, 2023 03:10Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) ameyapongeza makundi ya muqawama ya Palestina kwa ushindi wao mkubwa katika mapigano ya hivi karibuni na utawala haramu wa Kizayuni wa Israe ambayo yalimalizika tu baada ya Israel kukubali masharti yao.
-
Sisitizo kuhusu utambulisho wa ubaguzi wa rangi wa utawala wa Kizayuni wa Israel
May 29, 2023 07:46Mjukuu wa Nelson Mandela, marehemu kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, ameashiria jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika ardhi zao zilizoghusubiwa na kusema: “Wapalestina wanahitaji kuungwa mkono kivitendo kwa ajili ya kupata uhuru.”
-
China yaitaka Israel iache chokochoko, uporaji wa ardhi za Wapalestina
May 25, 2023 23:50China imeutaka utawala haramu wa Israel ukomeshe mara moja tabia yake ya uchokozi, kuchochea taharuki na kupora ardhi na rasilimali za Wapalestina hasa katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.