-
Tunisia yabadilisha jina la vituo vya TAXI na kuita Quds
Dec 15, 2017 00:48Chama cha wamiliki wa TAXI nchini Tunisia kimebadilisha jina la vituo vyake na kuviita Quds kama njia ya kulalamikia uamuzi wa Marekani wa kuitambua rasmi Quds kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Hamas: Hakuna nchi inayoitwa 'Israel' hata mji mkuu wake uwe 'Quds'
Dec 14, 2017 12:31Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, hakuna dola linaloitwa Israel hata mji mkuu wake uwe Quds tukufu.
-
Mwakilishi wa Mayahudi katika bunge la Iran: Hatua ya Trump ya kuitambua Quds mji mkuu wa Israel ni ubaguzi wa kimbari
Dec 14, 2017 12:29Mwakilishi wa jamii ya wachache ya Mayahudi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya rais wa Marekani ya kuitangaza Baitul Muqaddas mji mkuu wa utawala wa Kizayuni ni ubaguzi wa kimbari.
-
Erdogan: Israel ni dola vamizi na la kigaidi
Dec 13, 2017 12:43Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa, kuwa na nguvu na kumiliki silaha si dalili kuwa Marekani ina nguvu, na maamuzi yake yatasababisha matatizo makubwa katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Jumuiya ya NAM yakosoa hatua ya Marekani dhidi ya Quds
Dec 13, 2017 11:55Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) imekosoa vikali hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitambua Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Bunge la Iran: Quds ni kibla cha kwanza cha Waislamu na ni ya Umma wote wa Kiislamu
Dec 12, 2017 12:56Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, wamesema uamuzi wa Rais wa Marekani kutambua Quds Tukufu (Jerusalem) kama mji mkuu wa utawala bandia wa Israel ni dalili ya wazi kabisa ya kutokuwa na utambulisho utawala huo wa Kizayuni.
-
Jenerali Qassem Soleimani: Iran iko tayari kuvisaidia vikosi vya Muqawama vya Palestina kwa kila hali
Dec 12, 2017 12:48Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kutoa msukumo na kuvisaidia kwa kila hali vikosi vya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina.
-
Rais Rouhani kushiriki mkutano wa dharura wa OIC, Quds ndiyo ajenda kuu
Dec 12, 2017 04:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo anaelekea Uturuki kwa shabaha ya kushiriki katika kikao cha dharura cha viongozi wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) nchini Uturuki.
-
Trump, White House watengwa kutokana na uamuzi dhidi ya Quds
Dec 12, 2017 04:47Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema kitendo cha Donald Trump cha kuitangaza Quds ambayo ina Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa Israel imeifanya Ikulu ya White House na rais huyo wa Marekani watengwe kimataifa.
-
Rouhani: Mataifa ya Kiislamu yatazima njama ya Marekani na Israel
Dec 11, 2017 23:30Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema umoja, muqawama na mapambano ya Wapalestina na nchi nyingine za Kiislamu bila shaka yatapelekea kusambaratika kwa njama ya Marekani na utawala wa Kizayuni ya kuitambua Quds tukufu kuwa 'mji mkuu' wa utawala haramu wa Israel.