Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Israel imefeli kufikia malengo yake yote katika hujuma na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema 'nidhamu mpya ya dunia yenye uadilifu' itaibuka kutokana na damu za wananchi wa Palestina zilizomwagwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
Kinara wa upinzani nchini Liberia, Joseph Boakai ameibuka mshindi kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais, na kumbwaga Rais anayeondoka, George Weah aliyekuwa anagombea muhula wa pili.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria nafasi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika uongozi wa serikali halali katika eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuwa, vita dhidi ya kundi hilo la muqawama ni sawa na vita dhidi ya demokrasia.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mashambulizi yasiyo na kikomo ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yanashabihiana na vita vya kivamizi na kichokozi vya dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein dhidi ya Iran katika miaka ya 1980.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya hivi karibuni ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio juu ya vita vya Gaza ni mafanikio muhimu katika mkondo wa kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Marekani ya kulipigia kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusimamishwa mashambulizi na jinai za Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza ni dhulma maradufu dhidi ya Wapalestina na ubinadamu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameikumbusha jamii ya kimataifa kuwa ina wajibu wa kukomesha mgogoro katika wa Ukanda wa Gaza, ambapo Wapalestina wa eneo hilo wanakabililiwa na kila aina ya jinai kutoka kwa Wazayuni.
Rais Macky Sall wa Senegal amesaini dikrii ya kuivunja serikali yake, miezi michache kabla ya kumalizika hatamu yake ya uongozi.
Rais wa Iran amepuuzilia mbali madai ya madola ya Magharibi kwamba Jamhuri ya Kiislamu inataka kuunda silaha za nyuklia.