-
WHO yatahadharisha kuhusu hali iliyopo katika kambi za Waislamu wa Myanmar
Sep 25, 2017 11:01Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika kambi za wakimbizi huko Bangladesh unaotishia maisha ya Waislamu wa Rohingya wa Myanmar wapatao 436,000.
-
Waislamu Warohingya wanaendelea kuangamizwa kwa umati
Sep 23, 2017 04:34Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema ushahidi unaonyesha kuwa nyumba za Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar zinaendelea kuteketezwa katika jimbo la Rakhine.
-
Kuhusu Waislamu wa Rohingya, Suu Kyi ni mdanganyifu
Sep 20, 2017 21:57Wakimbizi Waislamu wa kabila la Rohingya wanaoishi makambini nchini Bangladesh wamesema hotuba aliyotoa Aun San Suu Kyi Waziri wa Mambo ya Nje na ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa Serikali ya Myanmar ni ya udanganyifu.
-
HRW: Jeshi la Myanmar liadhibiwe kwa kutekeleza maangamizi ya kimbari dhidi ya Waislamu
Sep 18, 2017 09:27Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetaka vikwazo vikali vya kimataifa viwekewe Jeshi la Myanmar kutokana na kampeni yake ya kutekeleza maangamizi ya kimbari dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.
-
Mkuu wa Majeshi Myanmar: Hatutasitisha mashambulizi yetu kuwalenga Waislamu wa Rohingya
Sep 18, 2017 03:31Licha ya ukosoaji na kulaaniwa na jamii ya kimataifa mauaji na ukandamizaji unaofanywa na askari wa serikali ya Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha magaidi kuwalenga Waislamu wa jamii ya wachache wa Rohingya, mkuu wa majeshi ya nchi hiyo amesisitiza kuwa jeshi hilo litaendeleza hujuma na mashambulizi hayo dhidi ya jamii hiyo ya Waislamu.
-
Mateso ya Waislamu wa Rohingya katika picha
Sep 17, 2017 06:31Hizi hapa chini ni baadhi ya picha zinazoonesha sehemu ndogo to ya matezo makubwa yanayowatesa Waislamu wa jamii ya Rohingya kutokana na ukatili na unyama wa kuchupa mipaka wanaofanyiwa na mabudha
-
India kuwafukuza wakimbizi Waislamu wa Myanmar wapatao 40,000
Sep 17, 2017 03:07Serikali ya India imewasilisha ombi katika Mahakama ya Juu ya nchi hiyo la kutaka kutimuliwa makumi ya maelfu ya wakimbizi Waislamu wa kabila la Rohingya, waliokimbilia usalama wao nchini humo kutokana na kushadidi mashambulizi ya jeshi la Myanmar likishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi yao.
-
Watafiti: Waislamu wa Rohingya waliofanikiwa kufika Bangladesh wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia
Sep 15, 2017 09:39Wafanyakazi wa misaada ya kibinaadamu nchini Bangladesh wameviambia vyombo vya habari kwamba Waislamu wa Rohingya waliofanikiwa kufika nchini humo, wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia kutokana na mateso ya kimwili waliyoyashuhudia nchini Myanmar kutoka kwa askari wa serikali ya nchi hiyo.
-
FAO: Waislamu laki moja Warohingya walioko Bangladesh wanahitajia msaada wa haraka wa chakula
Sep 15, 2017 00:03Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, Waislamu laki moja wa jamii ya Rohingya waliowasili nchini Bangladesh wanahitajia msaada wa haraka wa chakula.
-
UN yaeleza wasi wasi wake kuhusu wimbi la wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh
Sep 09, 2017 03:15Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeeleza wasi wasi mkubwa lilionao kutokana na kuendelea kumiminika idadi kubwa ya wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Bangladesh.