-
Lukashenko: Russia yakamilisha zoezi la kuikabidhi Belarus shehena ya silaha za nyuklia za kitaktiki
Dec 26, 2023 08:08Rais wa Belarus amesema kuwa Russia imekamilisha zoezi la kukabidhi Belarusia shehena ya silaha za nyuklia za kitaktiki ambazo zimetumwa nchini humo kwa lengo la kukabiliana na mashambulizi yoyote yanayoweza kutekelezwa na Mungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato).
-
Russia: Bila usitishwaji vita azimio la Baraza la Usalama halitakuwa kwa manufaa ya Gaza
Dec 26, 2023 03:30Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza katika taarifa kwamba azimio la hivi karibuni la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukanda wa Gaza halitaathiri hali ya ukanda huo, na kwamba kuna udharura wa kutekelezwa usitishaji vita katika ukanda huo haraka iwezekanavyo.
-
M’membe: Vikwazo vya Magharibi vimezikurubisha pamoja Russia, Afrika
Dec 25, 2023 07:12Rais wa Chama cha Kisoshalisti cha Zambia amesema nchi za Magharibi zinaziburuza nchi nyingine duniani kuingia vitani huku zikipora rasilimali zao.
-
Azimio la Baraza la Usalama kuhusu Gaza: Ni hatua ya lazima lakini haitoshi
Dec 23, 2023 04:48Ijumaa ya jana, Desemba 22, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuongeza misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza bila kutoa wito wa kusitishwa mapigano. Marekani na Russia, wanachama wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama, hazikulipigia kura azimio hilo. Wajumbe wengine 13 wamelipigia kura ya ndiyo.
-
Kuimarika uhusiano wa Russia na China, changamoto kubwa kwa mfumo wa Magharibi duniani
Dec 23, 2023 01:11Katika ziara yake nchini China, Waziri Mkuu wa Russia amesema kuimarishwa uhusiano wa pande mbili ni kwa manufaa ya Moscow na Beijing.
-
Iran yakosoa msimamo wa Russia kuhusu visiwa vitatu vya Jamhuri ya Kiislamu
Dec 22, 2023 22:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Russia kwamba, Tehran haiwezi kufanya majadiliano na mashauriano yoyote juu ya mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kujiandikisha Putin kwa ajili ya uchaguzi wa Russia 2024
Dec 19, 2023 23:07Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amethibitisha hhatua ya kwenda Rais Vladimir Putin wa Russia katika Kamati Kuu ya Uchaguzi ya nchi hiyo na kujiandikisha kama mgombea kwa muhula ujao wa urais, ambao utafanyika katikati ya Machi 2024. Putin amewasilisha stakabadhi zinazohitajika ili kujiandikisha kuwa mgombea urais.
-
Sisitizo la Putin la kutoziami nchi za Magharibi
Dec 18, 2023 23:04Siku ya Jumapili, Rais Vladimir Putin wa Russia alikiri katika hotuba isiyokuwa ya kawaida kwamba ni makosa kuzidhania vizuri na kuzitegemea nchi za Magharibi na kufikiria kuwa Russia haina tofauti na nchi hizo. Alisema: Nilidhani kimakosa kuwa hakungekuwepo mzozo kati ya Russia na nchi za Magharibi na kwamba ulimwengu ulikuwa umebadilika.
-
Russia: Wamagharibi hatimaye wataondoka Ukraine
Dec 12, 2023 00:05Mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Kigeni ya Russia amesema: "Utawala kibaraka wa Kyiv, ambao ni ngeni kwa watu wengi wa Ukraine na umetekeleza mauaji ya umwagaji damu huko Donbass, Odessa na miji na vijiji vingi vya nchi hiyo, hatimaye utaachwa na kutupiliwa mbali na Wamagharibi."
-
Rais wa Iran akiwa safarini Russia asisitiza kusitishwa jinai za Israel dhidi ya Gaza
Dec 07, 2023 23:49Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kusitishwa mara moja jinai za Israel za "mauaji ya kimbari" dhidi ya Wapalestina Ukanda wa Gaza.