Katibu Mkuu wa Arab League aelekea Russia kwa mazungumzo
(last modified Mon, 09 Oct 2023 02:34:23 GMT )
Oct 09, 2023 02:34 UTC
  • Katibu Mkuu wa Arab League aelekea Russia kwa mazungumzo

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amefanya ziara mjini Moscow Russia kwa ajili ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuhusu masuala mbalimbali.

Jamal Rushdi Msemaji wa Ahmed Abul Gheit Katibu Mkuu wa Arab League amethibitisha kuwa Abul Gheit yuko ziarani Moscow mji mkuu wa Russia kufuatia mwaliko wa Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo. 

Jamal Rushdi ameeleza kuwa, pamoja na mambo mengine, Abul Gheit amekuwa na mazungumzo ya kina na Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia kuhusu masuala ya pande mbili yakiwemo masuala ya kikanda na kimataifa khusuan mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza.  

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ametaka kusitishwa haraka iwezekanavyo mashambulizi ya  utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza. 

Wizara ya Afya ya Palestina jana ilitangaza kuwa, Wapalestina 313 wameuliwa shahidi na wengine 1990 kujeruhiwa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika maeneo ya raia huko Ghaza. 

Wizara hiyo imeongeza  kuwa, timu za madaktari na wafanyakazi wa huduma ya afya wa Palestina wanaendelea kufanya kila wawezalo ili kuwanusuru makumi ya majeruhi wa Kipalestina wenye hali mbaya ambao wako katika vyumba vya upasuaji na katika kitengo cha uangalizi maalumu. 

Juzi Jumamosi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilishambuliwa kwa mamia ya maroketi na makombora maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ikiwemo Tev Aviv, Ashdod na Ashkelon.

Kimbunga cha Al Aqsa dhidi ya Wazayuni