Russia yaharibu mfumo wa M777 wa Marekani huko Ukraine.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuharibu mfumo wa M777 wa Marekani na wa Crab katika operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine.
Sambamba na takwa la mara kwa mara la Ukraine la kujiunga na NATO na kupokea misaada ya dola milioni kadhaa kutoka nchi za Magharibi na kufuatia harakati za hivi karibuni za nchi za Magharibi karibu na mpaka wa Russia, Rais Vladimir Putin nchi hiyo mnamo Februari 24, 2022 akijibu ombi la usaidizi wa kijeshi kutoka kwa wakuu wa Donetsk na Luhansk mashariki mwa Ukraine aliamuru mashambulizi ya kijeshi katika eneo la Donbas. Baada ya hapo, wapiganaji wa Russia, walilenga vifaru na mifumo ya makombora ya jeshi Ukraine.
Rais Putin alisisitiza kuwa shambulio hilo lilifanyika kwa shabaha ya kuitenga na kuipokonya silaha Ukraine.
Rais wa Russia pia alikuwa ameonya kuwa hatua ya nchi za Magharibi ya kutuma silaha na mamluki nchini Ukraine zitasababisha umwangaji damu mkubwa nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilitangaza katika taarifa jana, kwamba katika saa 24 zilizopita zaidi ya wanajeshi 570 wa Ukraine wameuawa au kujeruhiwa huko Kopyansk, Zaporizhia, Donetsk, na Krasnolimansk na makombora manne ya Ukraine kuzuiliwa.
Vita vya miezi 20 nchini Ukraine pamoja na athari zake mbalimbali za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni bado zinaendelea kwa nchi za Magharibi kutuma silaha nchini humo.
Nchi za Ulaya na Magharibi, na hasa Marekani, kwa kuzidisha mashinikizo na kuiwekea Russia vikwazo si tu kwamba hazijachukua hatua ya kusimamisha vita bali zinaendelea kuchochea moto wa mgogoro kwa kutuma silaha nyepesi na nzito kwa Kyiv.
Maafisa wa Russia na baadhi ya wataalamu wa habari wa nchi za Magharibi wamevitaja vita vya Ukraine kuwa ni vita vya niaba kati ya Magharibi na Urusi.
Russia imekuwa ikisema mara kwa mara kuwa kupeleka nchi za Magharibi silaha nchini Ukraine kutarefusha mzozo huo na kupelekea kutotabirika matokeo yake.